Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.

BENKI  ya CRDB imeamua kuadhimisha siku ya Mtoto wa Afrika mwaka huu kwa kutoa elimu kwa wazazi kuhusiana na  masuala mbalimbali yanayohusu mtoto ili kuweza kuwajenga vizuri katika malezi.

Siku ya Mtoto Afrika kila mwaka yanadhimishwa Duniani huku Benki ya CRDB  ikiadhimisha kwa mwaka wa tano mfululizo ikiwa ni muendelezo wa kuhakikisha watoto na kuwaelimisha wazazi watakaofika katika matawi ya benki huyo..

Akizungumza na waandishi wa habari, MkurugenzI Mtendaji wa CRDB Charles Kimei amesema kuwa wao kama beki ya CRDB wataadhimisha siku ya mtoto wa Afrika katika kila tawi kwani ni siku muhimu kwa kila mtoto nchini kwetu.

"Tutaadhimisha siku ya mtoto Afrika nchini kwetu katika kila tawi la benki yetu pia itakuwa ni siku muhimu sana na kuienzi kwa kuelimisha wazazi masuala mbalimbali ya watoto,"alisema Kimei.

Kimei amesema kuwa,kuanzia kesho itakuwa ni wiki ya ya mtoto wa Afrika katika benki yao na watatoa elimu mbalimbali, kuelimisha wazazi masuala ya watoto pamoja na kuwahamasisha kufungua akaunti ya watoto ya Junior Jumbo.

Mbali na kuwa na elimu mbalimbali zinazohusu watoto, kila tawi la CRDB limejipanga kuhakikisha linatoa huduma nzuri kwa wateja watakaokuja siku ya kesho na wiki nzima kiujumla na hivyo ni katika kuboresha maisha ya mtoto wa kesho.

"Kuwa na wiki hii itakayokuwa inaadhimisha siku ya mtoto wa Afrika na wazazi watapewa elimu kwa watoto wao, pia CRDB wamelenga zaidi katika kusaidia mazingira ya watoto kupitia nyanja ya elimu  na kufanya hivyo ni kuboresha maisha ya mtoto wa kesho,"
amesema Kimei.

Amemalizia kwa kusema kuwa wateja watakaojitokeza ndani ya wiki ya mtoto wa Afrika katika matawi ya benki ya CRDB watahudumiwa kipekee na zaidi amewaomba kwenda kwa wingi kupata elimu mbalimbali kuhusu watoto na kuwafungulia akaunti kwa manufaa ya baadae.

MkurugenzI Mtendaji wa CRDB Charles Kimei akizungumza na waandishi wa habari kuelekea siku ya Mtoto wa Afrika itakayoazimishwa siku ya kesho na wao kama CRDB wataiadhimisha kwa wiki nzima ili kutoa elimu  kwa wazazi kuhusiana na  masuala mbalimbali yanayohusu mtoto ili kuweza kuwajenga vizuri katika malezi.
Waandishi wa habari wakimsikiliza MkurugenzI Mtendaji wa CRDB Charles Kimei.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...