WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali imeadhimia kupambana vilivyo dhidi ya biashara haramu ya dawa za kulevya na kuhakikisha inakuwa historia nchini.

Pia ametoa wito kwa wazazi wote nchini waendelee kufuatilia nyendo za watoto ili wasijiingize kwenye mtego wa dawa za kulevya na wala wasisubiri vijana wao waanze kutumia.

Ametoa kauli hiyo leo (Alhamisi, Juni 29, 2017) kwenye maadhimisho ya Kitaifa ya Siku ya Kupiga Vita Dawa za Kulevya Duniani, iliyoadhimishwa mjini Dodoma.

Kufuatia hali hiyo Waziri Mkuu amesema Serikali imejidhatiti kuhakikisha kuwa uzalishaji, usambazaji na matumizi ya dawa za kulevya unadhibitiwa kikamilifu nchini.

Amesema katika kutimiza azma hiyo, ambayo pia inaelekezwa na Ilani ya Uchaguzi ya CCM, Serikali ilifanya mabadiliko ya Sheria ya Dawa za Kulevya kwa kuanzisha chombo cha kisheria cha kupambana na biashara hiyo, ambayo imeongeza adhabu kwa wanaoshiriki.


Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akihutubia katika Maadhimisho ya Kitaifa ya Siku ya Kupiga Vita Dawa za Kulevya Duniani kwenye uwanja wa Nyerere mjini Dodoma Juni 29, 2017.
Balozi wa Uingereza Nchini, Sarah Cooke akizungumza katika Maadhimisho ya Kitaifa ya Siku ya Kupiga Vita Dawa za Kulevya Duniani kwenye uwanja wa Nyerere mjini Dodoma Juni 29, 2017
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama dawa mbalimbali za kulevya katika maonyesho yaliyokwenda sambamba na Maadhimisho ya Kitaifa ya Siku ya Kupiga Vita Dawa za Kulevya Duniani kwenye uwanja wa Nyerere mjini Dodoma Juni 29, 2017
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiweka jiwe la Msingi la Kituo cha Kutoa Huduma kwa Waathirika wa Dawa za Kulevya mjini Dodoma Juni 29, 2017. Kushoto ni Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu na kulia ni Kamishina Mkuu wa Mamlaka ya Kuzuia na Kupambana na Dawa za Kulevya, Rogers Sianga .

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...