Taasisi ya kupambana na kuzuia Rushwa nchini (TAKUKURU),imewafikisha Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu watu wawili James Rugemalira (Pichani kushoto) na Harbinder Seth Sigh (Pichani kulia) kwa tuhuma ya kesi ya Uhujumu Uchumi.
Akizungumza mapema leo mchana jijini Dar Es Salaam,Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa nchini (TAKUKURU), Valentino Mlowola amesema kuwa Mmiliki wa VIP Engineering and Marketing, James Rugemalira na Mmiliki wa Kampuni ya IPTL, Habirnder Seth wamefikishwa mahakama ya Kisutu leo mchana kwa kosa la kuhujumu uchumi pamoja na makoasa mengine yanayofanana na hayo.
Mlowola amesema kuwa watuhumiwa hao wameshafikishwa mahakamani kwa kosa la kuhujumu uchumi pamoja na makosa yanayofanana na hayo,akaongeza kusema kuwa TAKUKURU wamechunguza shauri hilo kwa muda mrefu na sasa imefika wakati kuwapeleka mahakamani watuhumiwa hao kujibu mashtaka yao.
Mlowola ametoa Wito kwa wananchi kutambua kuwa serikali ina nia njema na dhati kabisa ya kuwapa Maisha bora Watanzania,hivyo hakuna budi wale wote wanaotuhumiwa kwa makosa mbali mbali watafikishwa mbele ya vyombo vya sheria.
Kabla ya vigogo hawa wawili kufikishwa mahakamani leo, baadhi ya watumishi wa TANESCO tayari walishtakiwa kufuatia tuhuma za kupokea fedha kutoka kwa Mkurugenzi wa Kampuni ya VIP Engeneering and Marketing ambaye pia alikuwa Mkurugenzi wa kampuni ya kufua umeme ya Independent Power Tanzania Ltd (IPTL), James Rugemalira.
Kwa picha zaidi na habari kamili BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...