THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

BULEMBO AMALIZA ZIARA WILAYA 47 ZA MIKOA SABA, JOTO LAKE LASABABISHA CHADEMA 376 KUTIMKIA CCM

Na Bashir Nkoromo

Hatimaye Mjumbe wa kamati Kuu ya CCM, Mwenyekiti wa Jumuia ya Wazazi na Mbunge wa Kuteulia na Rais Alhaj Abdallah Bulembo, amemaliza ziara yake ya Kichama akiwa amefanikiwa kutembelea mikoa saba na jumla ya Wilaya 47 za mikoa hiyo.

Katika ziara hiyo ambayo alianza May 26, 2017, aliihitimisha jana, Juni 10, 2017 katika mkoa wa Geita, ziara ikiwa imechukua zaidi ya wiki mbili, ambapo mkoa wa kwanza kufanya ziara hizo uliuwa Dar es Salam na badaye kuendelea katika mikoa ya Dodoma, Manyara, Tabora, Kigoma, Kagera na Geita ambao ndio mkoa aliomalizia.

Alhaj Bulembo katika ziara hiyo ambayo haikuhusu Jumuia yake ya Wazazi Tanzania, bali ya Kichama zaidi ilikuwa mahsusi kwa kuagizwa na Bosi wake, Mwenyekiti wa CCM Rais John Magufuli, kwa lengo la kutoa shukrani kwa wana CCM kufuatia kura nyingi walizompa hadi kukipatia Chama Cha Mapinduzi kura nyingi wakati wa Uchaguzi Mkuu uliofanyika Oktoba 2015.

Hata hivyo Bulembo anasema, Shukrani hizo, ni za awali kwa kuwa Mwenyekiti Mwenyewe Rais Dk. John Magufuli atafanya ziara rasmi kutoa shukrani.
Mjumbe wa kamati Kuu ya CCM Alhaj Abdallah Bulembo akisiriki kuapa wakati wanachama wapya waliohamia CCM kutoka Chadema walipokuwa wakiapa na kuungwa mkono na wanachama wote katika kiapo hicho
Wanachama wapya wa CCM wakiapa
Wanachama wa CCM wapya wakiapa huku wakiungwa mkono na wanachama wote waliokuwa ukumbini, kula kiapo hicho
Alhaj Bulembo akimvalisha kofia mmoja wa wanachama hao wapya