Kwa mara ya kwanza kampuni ya Candy and Candy imeanzisha Application mpya inayojulikana kama NIKO HUB ambayo ni mkombozi wa wafanyabiashara wengi na watumiaji wa mtandao huo.NIKO HUB inajihusisha na mambo yote yanayohusu vyakula,vinywaji na filamu (movies).

Lengo kubwa la NIKO HUB ni kunyanyua wafanyabiashara wakubwa na wadogo kwa kupanua soko lao na kujiongezea kipato zaidi zaidi na kumuondolea usumbufu mteja wakati anapohitaji huduma ambapo Aplication hii inamfanya mteja kuagiza bidhaa na kuletewa mahali alipo kikubwa anachotakiwa kufanya ni kupakua Aplication hii kwenye Google Play bure na kisha anaanza kuitumia kwenye simu yake.

NIKO HUB inafanya kazi mahali popote ulipo katika bara la Afrika na popote unapoenda huhitaji kupakua Aplication nyingine bali unaendelea kutumia ileile, Aplication hii pia inabadili lugha kulingana na lugha inayotumika katika nchi husika kwa mfano Tanzania inapatikana kwa kiswahili lakini ukienda kwenye nchi za kiarabu zilizoko Afrika itakuletea lugha ya kiarabu na ukienda nchi inayotumia lugha ya kifaransa itafanya hivyo pia N.K.

Jambo kubwa ni kwamba NIKO HUB pia imeandaa tamasha litakalojulikana kama NIKO HUB EAT OUT FESTIVAL ambalo litafanyika siku ya sikukuu ya Eid na hakutakuwa na kiingilio kwa washiriki ambapo litashirikisha wajasiriamali mbalimbali wanaojihusisha na uuzaji wa vyakula mbalimbali na vinywaji.

Mkurugenzi wa Kampuni ya Candy And Candy Bw. Joe Kariuki akizungumza na waandishi wa habari kwenye ukumbi wa Idara ya Habari Maelelzo leo wakati akitambulisha Aplication yake mpya kwa ajili ya kuuza Vyakula, Vinywaji na Filamu Movie leo, kushoto ni Meneja wa kampuni hiyo Bi Hasna Mwishehe.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Candy And Candy Bw. Joe Kariuki akionyesha Aplication hiyo jinsi inavyofanya kazi wakati akizungumza na waandishi wa habari kwenye ukumbi wa Idara ya Habari Maelelzo leo wakati akitambulisha Aplication yake mpya kwa ajili ya kuuza Vyakula, Vinywaji na Filamu Movie leo, kushoto ni Meneja wa kampuni hiyo Bi Hasna Mwishehe.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Candy And Candy Bw. Joe Kariuki akizmpigia simu mmoja wa wamiliki wa mgahawa ulioko Sinza na kuagiza chakula ili aletewe alipo wakati akitambulisha Aplication yake mpya kwa ajili ya kuuza Vyakula, Vinywaji na Filamu Movie leo, kushoto ni Meneja wa kampuni hiyo Bi Hasna Mwishehe.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...