Na Baltazar Mashaka, Mwanza

Katibu wa Chama Cha Mapinduzi wa Mkoa wa Mwanza Bw. Raymond Mwangwala amesema kuwa uchaguzi wa chama hicho wa mwaka huu umelenga kuwapata viongozi bora watakaokivusha kwenye Uchaguzi wa Serikali za Mitaa wa mwaka 2019 na Uchaguzi Mkuu wa 2020.

Ameonya kuwa wana CCM watakaobainika kutumia rushwa ili wachaguliwe na watakaopokea rushwa hiyo wote watashughulikiwa kwa taratibu zilizowekwa.

Bw. Mwangwala alitoa kauli hiyo juma hili wakati akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake, ambapo aliomba ushirikiano wa wanahabari hao katika utekelezaji wa majukumu yake.

Alisema CCM mpya ya “hapa kazi tu” haitamchekea mtu yeyote mwenye kupanga kukiharibu chama hicho kwa namna anayotaka na haitakuwa tayari kupokea mamluki wanaojiunga nayo kwa maslahi binafsi badala ya wananchi na wana CCM.

Katibu huyo alieleza kuwa ili wapatikane viongozi waadilifu watakaoinua mapato ya CCM na kukisaidia chama hicho tawala kwenye uchaguzi wa 2020, wanachama wenye sifa na uwezo wakachukue fomu ili wapigiwe kura kwani ndio watakaokifikisha kwenye uchaguzi huo na kukiwezesha kupata kura za ushindi za urais, ubunge na udiwani.

Bw. Mwangwala alisisitiza kuwa watakaotumia rushwa hawatapitishwa kugombea nafasi wanazoomba kwani wanatakiwa viongozi wa kusimama na kuielezea CCM badala ya mamluki.

Hata hivyo katibu huyo alisema chama hicho kinafanya uhakiki wa mali zake kuanzia ngazi ya matawi, wilaya hadi mkoa ili zitambulike na kufahamu mapato yake yalikuwa yanatumikaje.

“Zipo mali watu walikuwa wakizutumia vibaya kutokana an mikataba mibovu iliyopo, watakaobainika kwenye zoezi la uahkiki watashughulikiwa na wapo waliodiriki kuziuza mali hizo na kuzigeuza shamba la bibi,
“Tunataka tujue mali zetu zilipo na zingine zilizotelekezwa tuzijue na mapato yake yanatumikaje.Ifikapo Julai mwaka huu zote ziwe na hati,”alisema. 
Katibu wa CCM wa Mkoa wa Mwanza Bw. Raymond Mwangwala akizungumza na wanahabari ofisini kwake katikati ya juma hili.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...