Na Fredy Mgunda, Mufindi.
Mbunge wa jimbo la Mafinga Mjini mh Cosato Chumi amefanikiwa kutatua tatizo la vitanda katika shule ya sekondari Isalavanu iliyopo Kata ya Isalavanavu kwa kutoa vitanda 35 ikiwa lengo la kuendelea kuboresha na kuinua elimu ya shule hiyo.
Akizungumza wakati wa kukabidhi vitanda hivyo alisema kuwa ameamua kufanya hivyo kutokana na ziara yake akiyofanya wiki kadhaa zilizopita wakati alipozitembelea shule mbalimbali za jimbo la Mafinga Mjini kujua changamoto na kuanza kuzitafutia ufumbuzi changamoto hizo.
"Niligombea ubunge wa jimbo la Mafinga kwa lengo la kuleta maendeleo ndio maana Leo nipo hapa katika shule ya sekondari ya Isalavanu kuanza kuinua elimu ya shule hii kwa kuboresha miundombinu ya shule na baadae nitatu changamoto nyingine"alisema Chumi
Chumi aliwataka wanafunzi wa shule ya Isalavanu kusoma kwa bidii ili kuleta matokeo chanya katika jimbo la Mafinga Mjini kwa lengo la kumuongezea kasi ya kutafuta wafadhili wa kusaidia kuleta maendeleo katika jimbo la Mafinga.
" Kwa kweli najitahidi kutafuta wafadhili wa kusaidia kutatua changamoto za jimbo la Mafinga Mjini lakini wananchi wangu na ninyi wanafunzi mnatakiwa kunipa matokeo chanya na kufanya maendeleo yenu ya mtu moja moja na vikundi pia natamani siku moja kila sekta niwakute watu kutoka jimbo la mafinga Mjini" alisema Chumi

Mbunge wa jimbo la Mafinga Mjini mh Cosato Chumi akimkabidhi vitanda 35  Mwenyekiti wa halmashauri ya Mji wa Mafinga ndg Charles Makoga kwa ajili ya kutatua changamoto zilizokuwa zinawakabili wanafunzi wa shule ya Isalavanu iliyopo katika Wilaya ya Mufindi
Mbunge wa jimbo la Mafinga Mjini Cosato Chumi akiwa sambamba n wanafunzi wa shule ya sekondari y Isalavanu pamoja na Mwenyekiti wa halmashauri ya Mafinga Mjini Charles Makoga
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...