THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

Dau nono la Milioni 10 za Biko laenda kwa Junior Pesambili wa Makete

DAU nono la Sh Milioni 10 linalotolewa kama zawadi ya droo kubwa ya Mchezo wa Kubahatisha wa Biko limeenda kwa Junior Ashery Pesambili wa Lupela, Makete, mkoani Njombe, ikiwa ni mwendelezo wa kugawa fedha kwa washindi wake ikitokana na matokeo ya droo ya 11 iliyochezeshwa jana Jumapili.

Droo hiyo iliyochezeshwa jana iliendeshwa na Balozi wa Biko Kajala Masanja, akishirikiana na mwakilishi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Bakari Maggid. Akizungumza katika droo hiyo jana, Meneja wa Huduma kwa Wateja wa Biko, Grace Kaijage, alisema wamedhamiria kugawa mamilioni kwa washindi wao wanaocheza mchezo wa Biko uliozidi kushika kasi katika kona mbalimbali nchini Tanzania.
Alisema tayari wameshafanya droo 11 kubwa ambapo watu mbalimbali wameendelea kupokea fedha zao ikihusisha vijana bila kusahau mzee Stanley Kapondo naye aliyekuwa miongoni mwa Watanzania waliovuna zawadi mbalimbali kutoka Biko.

“Kucheza Biko mara nyingi zaidi ndio nafasi kubwa ya kuibuka na ushindi, hivyo ni wakati wa Watanzania kucheza mara nyingi ili washinde, ukizingatia kuwa mbali na donge nono la Milioni 10 linalotolewa Jumatano na Jumapili, pia mtu anaweza kushinda zawadi mbalimbali kuanzia Sh 5,000, 10,000, 20,000, 50,000, 100,000, 500,000, 1,000,000, huku droo ya Jumatano hii ikitoa Sh Milioni 20 kwa mshindi wake kama ilivyokuwa Jumatano iliyopita.

“Mchezo wetu unachezwa kwa njia ya ujumbe mfupi wa maandishi kwa kufanya miamala kwenye simu za Tigo Pesa, M-Pesa na Airtel Money ambapo utakapoingia kwenye kipengele cha Lipa Bili au lipa kwa Mpesa, mshiriki wetu ataingiza namba ya kampuni 505050 na baadaye kuweka namba ya kumbukumbu 2456, huku akianzia kucheza kwa Sh 1000 au zaidi,” Alisema Grace.


Balozi wa Biko Tanzania, Kajala Masanja, kulia akionyesha namba ya ushindi wa Sh Milioni ya mshindi wao wa Lupela, Makete,mkoani Njombe, Junior Ashery Pesambili aliyepatikana katika droo ya jana Jumapili. Kushoto ni mwakilishi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Bakari Maggid.

Balozi wa Biko Kajala Masanja akifurahia namba ya mshindi wa Sh Milioni 10 kutoka Makete, mkoani Njombe, droo iliyochezeshwa jana jijini Dar es Salaam.