THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

DC KASESELA AKESHA KUANZIA SAA MBILI ASUBUHI HADI SAA SITA USIKU MGODINI NYAKAVANGALA KUOKOA MAITI YA MCHIMBAJI

Na Fredy Mgunda, Iringa.

Mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela alilazimika kufanya kazi ya uokoaji wa maiti ya mchimbaji madini katika mgodi wa Nyakavangala bwana Vaspa nyenza mkazi wa Itengulinyi Kata ya Ifunda wilaya ya Iringa kwa takribani masaa kumi na nane

Kasesela alisema kuwa alianza kazi hiyo majira ya saa mbili asubuhi alipowasili katika mgodi huyo wa Nyakavangala lakini yeye,waandishi wa habari na viongozi wengine wa wilaya ya Iringa walijitahidi kuokoa mwili wa marehemu hadi majira ya saa sita usiku lakini zoezi hilo lilikuwa likiendelea

"Hadi saizi tumepiga dua zote lakini hali ngumu sijui nini kinaendelea katika hili shimo maana waokoaji kila wakiukaribia mwili wa marehemu miamba laini inavungika na kujaza udongo ndani ya shimo ndio maana mmeniona naangaika na ndugu wa marehemu kujaribu kusali huku na kule lakini hali ni ngumu hadi muda huu wa saa tano usiku"alisema Kasesela

Aidha Kasesela aliwataka ndugu wa marehemu na viongozi mbalimbali kuwa na subila wakati wanalishugulikia swala la kuokoa mwili wa mpendwa wao kwa kuwa wameshaukaria mahali ulipo.

"Ungalia tayari kichwa na kiwiliwili vimeshaonekana kwa hiyo tumebakiza sehemu ndogo tu naombeni tuwe wavumilivu kwa kuwa tuvumilia toka siku ya jumapili hadi usiku huu basi tuungane kumuombea mwenzetu ili tutoe mwili wake ukiwa salama" alisema Kasesela
Mkuu wa Wilaya ya Iringa Richard Kasesela akiwa katika mgodi wa nyakavangala uliopo katika Kata ya malengamakali Mkoani Iringa wakati wa Juhudi za kuuokoa mwili wa marehemu viskadi nyenza katika shimo alilosimama Mkuu huyo wa Wilaya.
Mkuu wa Wilaya ya Iringa Richard Kasesela akisaiadiana na wachimbaji madini katika mgodi wa nyakavangala ili kuokoa mwili wa marehemu Nyenza
Mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela alipokuwa akiwasili katika mgodi wa nyakavangala uliopo Kata ya malengamakali Mkoani Iringa.