Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.

Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga Filbert Sanga amewataka wanawake wa Wilaya hiyo kuachana na masuala ya utegemezi kwa wanaume na zaidi wajikite katika kujiendeleza kiuchumi kwa kuanzisha miradi midogo midogo ikiwemo kuanzisha vikundi vya ujasiriamali  ikiwa ni katika kutekeleza maagizo ya Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu ya kila Wilaya kuwa na vikundi vya kujiinua kiuchumi..

Amesema hayo wakati wa uzinduzi wa Jukwaa la Uwezeshaji wanawake lililofanyika jana na kuvikutanisha zaidi ya vikundi 30 kutoka Wilaya ya Mkuranga na kuelezea matatizo wanayokumbana katika vikundi vyao.

Sanga amewaambia kuwa wanawake bila kuwezeshwa wanaweza wakajiendeleza wenyewe kwani utakapomuelimisha mwanamk mmoja utakuwa umeelimisha watu wnegi sana.

"wanawake mkijiwezesha wenyewe mnaweza sio lazima muwezeshwe kwani tunachoamini ni kuwa ukimuelimisha mwanamke umeelimisha dunia kwani nyinyi ndiyo msingi mkubwa wa familia katika jamii zinazotuzunguka mtakapoamua kukaa na kutokujishughulisha basi hakutakuwa na msingi mzuri wa kizazi kijacho,"amesem Sanga.

Kwa upande wa Mwenyekiti wa Jukwaa la Uwezeshaji  WanawakeWilaya ya Mkuranga Mariam Ulega alisema kuwa anashukuru sana kwa Mkuu wa Wilaya kuja kuwazindulia jukwaa lao na cha zaidi kwa kuwa wameshapatikana viongozi wa Jukwaa hilo kwa wilaya ya Mkuranga na zaidi anaomba umoja na ushirikiano kutoka kwa wakina mama kutoka kata mbalimbali ili kufanya kazi kwa ushirikiano mkubwa.

Kabla ya kuzinduliwa kwa jukwaa hilo ulifanyika uchaguzi na kupatikana kwa Mwenyekiti Mariam Ulega. 
Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga Filbert Sanga akizindua Jukwaa la Uwezeshaji wanawake lililofanyika jana na kuwasihi wanawake kuachana na masuala ya utegemezi zaidi wanatakiwa kujiendeleza ili kujiinua kiuchumi na pia kuviendeleza vikundi vyao na kuvisajili ikiwa ni katika kutekeleza maagizo ya Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu ya kila Wilaya kuwa na vikundi vya kujiinua kiuchumi.
Mwenyekiti wa Jukwaa la Uwezeshaji Wanawake Wilaya ya Mkuranga Mariam Ulega akizungumza na wakina mama wa wilaya hiyo kutoka kata mbalimbali kuhusiana na kuviendeleza vikundi vyao kwa ajili ya kuacha kuwa tegemezi kwa wanaume ikiwa ni katika kutekeleza maagizo ya Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu ya kila Wilaya kuwa na vikundi vya kujiinua kiuchumi.


 Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga Filbert Sanga akipokea maandamano ya wakina mama wa Mkuranga wakati wa uzinduzi wa Jukwaa la Uwezeshaji wanawake lililofanyika jana na kuwasihi wanawake kuachana na masuala ya utegemezi zaidi wanatakiwa kujiendeleza ili kujiinua kiuchumi na pia kuviendeleza vikundi vyao na kuvisajili ikiwa ni katika kutekeleza maagizo ya Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu ya kila Wilaya kuwa na vikundi vya kujiinua kiuchumi.

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...