Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro amewataka wananchi wa kijiji cha Mwamagunguli kata ya Kolandoto manispaa ya Shinyanga kuacha kuchanganya siasa kwenye masuala maendeleo kwani inakwamisha shughuli za maendeleo na kusababisha kero katika jamii.

Matiro ameyasema hayo jana June 21,2017 baada ya kutatua mgogoro wa mradi wa maji ya kisima kirefu katika kijiji hicho ambapo viongozi wa eneo hilo kuanzia ngazi ya kitongoji hadi kata na wananchi walikuwa hawatumii maji hayo wakidai kuwa yana chumvi na hata yakitumika kupikia chakula yanakibadilisha na kuwa na rangi ya njano.

Kufuatia utata huo wa mradi huo ambao ujenzi wake ulikamilika tangu Mwaka 2014 kwa gharama ya shilingi milioni 294.6,Mkuu huyo wa wilaya aliamua kufika katika kijiji hicho ili kubaini ukweli wa madai ya wananchi hao.

Baada ya kufika katika kijiji hicho akiwa ameambatana na baadhi ya wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama wa wilaya hiyo pamoja na viongozi wa halmashauri ya manispaa ya Shinyanga walizungumza na wananchi wa eneo hilo ambao walisisitiza kuwa maji hayo hayafai mbele ya mkuu wa wilaya.

Mmoja wa wananchi hao,Shija Luhende aliuponda mradi huo wa maji mbele ya mkuu huyo wa wilaya akidai kuwa maji ya mradi huo wa kisima kirefu ukiyapikia kwenye ugali au wali chakula kinakuwa cha njano kutokana na kuzidi kwa chumvi hivyo hayafai kwa matumizi ya binadamu.

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga akiwa ameshikilia sahani yenye wali uliopikwa kwa maji yaliyokuwa yanadaiwa kuwa ukiyatumia kwa chakula,chakula kinabadilika na kuwa na rangi ya njano Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akizungumza na wakazi wa kijiji cha Mwamagunguli.
Wananchi wa kijiji hicho wakimsikiliza mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro 
Mmoja wa wananchi hao Shija Luhende akiuponda mradi huo wa maji mbele ya mkuu huyo wa wilaya kuwa maji yake ukiyapikia kwenye ugali au wali chakula kina kuwa cha njano kutokana na kuzidi kwa chumvi na hayafai kwa matumizi ya binadamu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...