Imeelezwa kuwa sababu kubwa inayochangia watoto kuendelea kunyanyaswa na kufanyiwa vitendo vya kikatili katika maeneo ya kanda ya ziwa ni jamii kukosa elimu kuhusu haki za watoto pamoja na kukosekana kwa ushirikiano pale kesi zinazopelekwa katika vyombo vya sheria.

Hayo yamesemwa leo June 16,2017 na Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro wakati wa maadhimisho ya siku ya Mtoto wa Afrika yaliyofanyika katika Viwanja vya Shycom Mjini Shinyanga.

Matiro alisema tatizo kubwa linalotokea wakati wa kutetea haki za watoto wanapofanyiwa ukatili ni kukosekana kwa ushirikiano wa jamii na wazazi pale kesi inapofika katika vyombo vya sheria ikiwemo mahakamani hivyo kusababisha kesi nyingi kufutika matokeo yake watoto wanaendelea kunyanyasika.

“Naomba tuweke mkazo zaidi katika elimu kwa jamii kuhusu haki za watoto,jamii ikibadilika tunaweza kumaliza tatizo la unyanyasaji wa watoto,wazazi wakielimika watajitokeza katika vyombo vya sheria kutoa ushahidi kwa vitendo vya kikatili wanavyofanyiwa watoto wao”,alieleza Matiro.

“Haki za watoto zinadidimizwaa sana kanda ya ziwa hasa mkoani Shinyanga kutokana na jamii kukosa elimu na kung’ang’ania mila na desturi zinazomgandamiza mtoto hususani mtoto wa kike hivyo mashirika na serikali tushirikiane kubadilisha fikra za jamii,wananchi wajue haki za watoto na wazilinde”,aliongeza Matiro.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akizungumza wakati wa maadhimisho hayo ambapo aliwataka watoto kusoma kwa bidii kwani elimu ni mkombozi wa maisha yao
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akiangalia bidhaa mbalimbali zilizotengenezwa na watoto waliopo katika kituo cha huduma ya watoto Shirika la Compassion katika kanisa la KKKT Shinyanga
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akiangalia masweta na nguo mbalimbali zilizotengenezwa na watoto hao.

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...