Na Dickson Mulashani

Mkuu wa wilaya Ilala Mh. Sophia Mjema amekipongeza Chuo cha St Mark (Chuo Kikuu Kishiriki Cha St Joseph) kwa jitihada za kutoa elimu bora kwa manufaa ya wilaya na Taifa kwa ujumla alipofanya ziara ya kikazi chuoni hapo mwishoni mwa juma.

Akiwasili chuoni hapo Mh. Sophia Mjema alikuwa ameambatana na ujumbe wa timu ya wataalamu katika ngazi mbalimbali a wilaya ya Ilala akiwemo Mratibu Mwadamizi wa Polisi, Mshauri wa Majeshi ya akiba, Mratibu wa Magereza, Mhandisi , Afisa uhamiaji, Afisa Elimu Taaluma, Afisa mipango miji, Afisa ustawi wa jamii, Afisa wa Benki ya NMB, Afisa Tarafa, Diwani pamoja na Mwenyekiti wa mtaa.

Akimkaribisha mgeni huyo, kaimu Mkuu wa Chuo Dr.Peter Kopweh alianza kwa kuelezea historia fupi ya chuo hicho kilichopo eneo la Buguruni Malapa jirani na shule ya msingi viziwi, kuwa ni sehemu ya Chuo Kikuu cha St. John’s chenye makao yake makuu mjini Dodoma ambacho kinatoa kozi katika ngazi astashada na shahada za sanaa katika elimu, utawala wa biashara, rasilimali watu, elimu na biashara pamoja na theolojia mathalani shahada ya uzamili katika elimu hili kwa ushirikiano na kampasi mama ya Dodoma.

Sambamba na ukaribisho huo Dr. Kopweh hakusita kuelezea Changamoto zinazokikabili chuo hicho zikiwemo za miundombinu ya barabara, usalama wa mali pamoja na wadau wake kadhalika suala la mipaka ambayo inaonekana kuingiliwa na wakazi wanaozunguka chuo hicho.
Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mh. Sophia Mjema akizungumza na wanajumuiya ya Chuo cha St. Mark kilichopo Buguruni Malapa alipofanya ziara ya kikazi chuoni hapo.Kulia kwake ni Makamu Mkuu wa Chuo Dr. Peter Kopweh na kushoto ni Mshauri wa majeshi ya akiba Chripin Makota.
Wanajumuiya ya Chuo cha St. Mark kilichopo Buguruni Malapa wakimsikilia Mh.Sophia Mjema alipofanya ziara ya kikazi chuoni hapo.
Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mh. Sophia Mjema akianza ziara kuzuru maeneo mbalimbali yaliyopo katika mazingira ya chuo cha St.Mark akiwa ameambatana na kamati ya ulinzi na usalama pamoja na timu ya wataalamu wa wilaya ya Ilala.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...