THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

Gadget

This content isn't available over encrypted connections yet.

DED MSALALA: MFUMO WA UHASIBU NA UTOAJI TAARIFA - FFARS NI TIBA YA HATI ZA MASHAKA KWENYE HALMASHAURI

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Msalala wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga Simon Berege ameupongeza mfumo mpya wa uhasibu na utoaji taarifa za fedha kwa ngazi ya kituo cha kutolea huduma ‘Facility Financial Accounting and Reporting System – FFARS na kueleza kuwa mfumo huo ni suluhusisho la hati zenye mashaka katika halmashauri mbalimbali nchini.

Mfumo wa FFARS unatekelezwa katika mikoa 13 kwenye halmashauri 93 kwa ushirikiano wa serikali na mradi wa Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma ‘ Public Sector Systems Strengthening – PS3’ unaofadhiliwa na Shirika la Maendeleo ya Kimataifa la Marekani (USAID) pamoja na Mradi wa Tuimarishe Afya ‘ Health Promotion and System Strengthening – (HPSS) unaofadhiliwa na watu wa Uswizi (Swiss Tropical and Public Health Institute). 

Akifungua mafunzo kuhusu mfumo huo kwa maafisa elimu kata na Waganga Wafawidhi katika vituo vya afya kutoka kata 18 za halmashauri ya Msalala,yaliyofanyika leo katika ukumbi wa Submarine Hotel mjini Kahama,Berege alisema mfumo wa FFARS ni mwarobaini wa tatizo la halmashauri kupewa hati zenye mashaka. 

Alisema mfumo huo utawezesha takwimu nyingi za halmashauri za wilaya kukusanywa kwa usahihi zaidi kutoka vituo vya kutolea huduma ambavyo vitakusanya na kuhifadhi taarifa za mapato na matumizi ya fedha za serikali kwa kutumia mfumo huo. 

“Takwimu ni tatizo la kitaifa,hivyo mfumo huu utasaidia kuondoa tatizo hili kwa kuongeza uwazi na umakini katika masuala ya uhasibu na utoaji taarifa za fedha”,alieleza Berege. “Halmashauri zimekuwa zikipata hati zenye mashaka kwa sababu uwekaji takwimu haupo vizuri,FFARS ni tiba ya hati zenye mashaka,pamoja na kuendelea kutumia njia za vitabu/makaratasi,ni vyema halmashauri zikawa tayari kutumia njia za ki- elektroniki katika utunzaji takwimu”,aliongeza Berege. 

Aidha alilishukuru Shirika la Maendeleo ya Kimataifa la Marekani (USAID) kwa kufadhili mradi huo na kuwataka watanzania kuutumia vizuri ili kuleta maendeleo katika halmashauri. 
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Msalala wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga Simon Berege akifungua kuhusu mfumo mpya wa uhasibu na utoaji taarifa za fedha kwa ngazi ya kituo cha kutolea huduma ‘Facility Financial Accounting and Reporting System – FFARS kwa maafisa elimu kata na waganga wafawidhi katika vituo vya afya kutoka halmashauri hiyo leo Alhamis June 8,2017 katika ukumbi wa Submarine Hotel mjini Kahama 
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Msalala Simon Berege akizungumza wakati wa kufungua mafunzo hayo 
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Msalala Simon Berege akifungua mafunzo hayo.Kushoto ni Mshauri wa kifedha kutoka PS3,Osoro Otieno,kulia ni Mratibu wa PS3 Halmashauri ya Msalala,Elikana Zabron .