Shirika linaloongoza katika kutoa huduma za malipo Direct Pay Online ni mdhamini wa maonyesho makubwa ya utalii na biashara kanda ya Afrika Mashariki ya KILIFAIR 2017. Maonyesho hayo yaliyofanyika katika uwanja wa Ushirika tarehe 2 hadi 4 mwezi Juni mwaka huu yalikusanya wafanyabiashara zaidi ya 300 kutoka Tanzania na nchi jirani na kuwa na wageni zaidi ya 3000 kutoka nje na ndani ya nchi. 

“Tunajivunia kuwa wadhamini wa kiwango hiki cha platinamu katika maonyesho makubwa kama haya. Hii ni fursa muhimu kwa kampuni yetu ya DPO kujitangaza kwa kazi kubwa tunayofanya ya kurahisisha malipo haswa kwa sekta ya safari,” alisema Mkurugenzi Mkuu wa DPO Eran Feinstein. 

Katika bidhaa zilizokuwa katika maonyesho kwende banda la DPO ni pamoja na huduma ya bure inayoitwa MarketPlace ambayo iko wazi kwa wafanyabiashara na wateja wote wa hoteli, safari, mawakala na maduka wa DPO wanaotumia tovuti hiyo na huduma nyingine kuuza bidhaa zao na pia kuwapatia fursa ya kujitangaza ulimwenguni bure. DPO pia ilionyesha jinsi ya kutumia programu ya DumaPay ambayo inawezesha wafanyabiashara kuwatoza wateja wao kutumia teknolojia inayosoma kadi kwa usalama mahali popote na muda wowote. Mteja huweza kulipa kupitia kadi au simu kwa sarafu wanayopendelea.  Waziri wa Maliasili na Utalii, Profesa Jumanne Maghembe (kulia) akimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa kampuni ya Direct Pay Online Group, Eran Feinsten (kushoto) jinsi wanavyotumia mfumo wa mawasiliano kutuma na kupokea fedha katika banda la kampuni hiyo katika maonesho ya Utalii na Viwanda ya Kili Fair yaliyofanyika kwenye uwanja wa Chuo cha Ushirika Moshi katikati ni Mkuu wa wilaya ya Moshi, Kippi Warioba.


Waziri wa Maliasili na Utalii,Profesa Jumanne Maghembe (kulia) akizungumza na maafisa wa kampuni ya Direct Pay Online, Kate Gathii (kushoto) ambaye ni Mkuu wa Masoko na Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa kampuni hiyo, Eran Feinsten (wa pili kushoto) alipotembelea banda la kampuni hiyo katika maonesho ya Utalii na Viwanda ya Kili Fair yaloyofanyika kwenye uwanja wa Chuo cha Ushirika Moshi kuanzia taerehe 2 Juni, wengine ni Mwenyekiti wa Bodi ya Utalii (TTB) Jaji Mstaafu Thomas Mihayo na Mkuu wa wilaya ya Moshi, Kippi Warioba. 

Waziri wa Maliasili na Utalii, Profesa Jumanne Maghembe (kulia) akikaribishwa na Mkuu wa Masoko wa kampuni ya Direct Pay Online, Kate Gathii (kushoto) alipotembelea banda la kampuni hiyo ambao ni platnimu sponsor wa maonesho ya Utalii na Viwanda ya Kili Fair yaliyofanyika kwenye uwanja wa Chuo cha Ushirika Moshi kuanzia tarehe 2 June. Wa pili kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa kampuni hiyo,Eran Feinsten,wengine ni Mwenyekiti wa Bodi ya Utalii (TTB) Jaji Mstaafu Thomas Mihayo na Mkuu wa wilaya ya Moshi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...