Na Mwamvua Mwinyi, Bagamoyo 

RAIS mstaafu wa awamu ya Nne ambae pia ni mkulima wa tunda la mnanasi ,dk.Jakaya Kikwete,amewataka wamiliki wa viwanda vya matunda kuacha kuwakandamiza wakulima kwa kununua matunda kwa gharama ya chini .

Amesema viwanda hivyo vinasaidia kupatikana kwa masoko ya ndani lakini vimekuwa havina uwiano wa gharama zinazolingana na maumivu anayoyapata mkulima.Aidha dk. Kikwete ameeleza kumekuwa na changamoto ya kushuka kwa soko kwa wakati mwingine hali inayokuwa ikisababisha wakulima kupata hasara kwa matunda kuoza yakiwa mashambani .

Akitoa taarifa ya shamba lake la mananasi lililipo Bago-Kiwangwa wilayani Bagamoyo ,wakati Mwenge wa Uhuru ulipokwenda kutembelea shamba hilo ,alisema kilimo cha matunda kina tija endapo utalima kisasa na kuwa na soko la uhakika .

Kikwete alieleza ,viwanda vya usindikaji matunda mbalimbali ,vinapaswa kumjali mkulima ambae amekuwa akipata shida na kutumia gharama kubwa kuandaa shamba .“Wakati utafika watakosa matunda ,kutokana na gharama yao hailipi ,wakulima wa matunda tushindwa kukubali kuuza kwa bei ya chini ambayo hailipi ” alifafanua .
Rais mstaafu wa awamu ya nne dk .Jakaya Kikwete akishika Mwenge wa Uhuru uliopita kutembelea shamba lake la mananasi lililopo Bago -Kiwangwa Bagamoyo .(Picha na Mwamvua Mwiny.
Rais mstaafu wa awamu ya nne dk .Jakaya Kikwete na mkewe mama Salma Kikwete wakikimbiza Mwenge wa Uhuru uliopita kutembelea shamba lake la mananasi lililopo Bago -Kiwangwa Bagamoyo .
 
Kongozi wa mbio za mwenge kitaifa Amor Hamad ,akizungumza baada ya kupata taarifa ya ujenzi ,wa kiwanda cha kusindika matunda cha sayona kilichopo Mboga – Msoga Chalinze ,kutoka kwa afisa uhusiano wa kampuni mama ya MMI ,Abubakar Mlawa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...