RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein ametoa wito kwa Baraza la Wauguzi na Wakunga la Zanzibar kusimamia vyema Sheria ya Baraza hilo sambamba na maadili kwa lengo la kuwahudumia vyema wananchi na kuzifanya huduma za afya zizidi kuimarika na kuendelea kuijengea sifa Zanzibar kama ilivyokuwa hapo siku za nyuma.

Dk. Shein, aliyasema hayo leo wakati alipokuwa na mazungumzo na Wajumbe wa Baraza la Wauguzi na Wakunga waliofika Ikulu mjini Zanzibar kwa ajili ya kujitambulisha kwa Rais wakiwa wameongozana na uongozi wa Wizara ya Afya chini ya Waziri wa Wizara hiyo Mahmoud Thabit Kombo.

Katika maelezo yake Dk. Shein aliwaeleza Wajumbe hao haja na umuhimu mkubwa wa kuipitia na kuisoma vyema vifungu vyote na hatimae kuifanyia kazi Sheria ya Baraza la Wauguzi na Wakunga la Zanzibar ya mwaka 2014 ili waweze kuliongoza vyema na kwa ufanisi zaidi Baraza hilo.

Dk. Shein, alisema kuwa iwapo Sheria hiyo itasimamiwa vyema  fani ya Uuguzi itaendelea kuwa na mafanikio makubwa sana hapa Zanzibar.

Alieleza matumaini yake makubwa kwa wajumbe hao ambao wamechaguliwa kutokana na kuwa kazi hiyo wanaiweza na kuwapongeza kwa kufanya mambo mengi tokea kuzinduliwa Baraza hilo lenye Wajumbe 13 Mrajis na wasaidizi wake wawili mmoja Pemba na mmoja Unguja mnamo mwezi June mwaka 2015.

Aidha, Dk. Shein alisisitiza suala zima la maadili ambalo ndio jambo muhimu katika fani yoyote duniani na kueleza kuwa katika fani ya Uuguzi suala la maadili ndio jambo la kulipa kipaumbele ili kuweza kutoa huduma nzuri ya afya kwa jamii.

BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...