THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

Gadget

This content isn't available over encrypted connections yet.

DMF, CBA BANK WASHIKIANA NA MPANGO WA TAIFA WA DAMU SALAMA KATIKA ZOEZI LA UCHANGIAJI DAMU, MBAGALA JIJINI DAR

Afisa Muuguzi kutoka Mpango wa Taifa wa Damu Salama, Cesilia Meela akiwatoa damu baadhi ya Wakazi wa eneo la Mbagala, Jijini Dar es salaam wakati wa zoezi la kuchangia damu lililofanywa na Taasisi ya Doris Mollel kwa kushirikiana na Benki ya CBA, iliyofanyika kwenye Kituo kikuu cha Mabasi, Mbagala Rangi Tatu, jijini Dar es Salaam jana. Jumla ya Units 106 zilipatikana.
Sehemu ya Wakazi wa eneo la Mbagala Rangi Tatu wakishiriki zoezi la uchangiji damu, llililofanywa na Taasisi ya Doris Mollel kwa kushirikiana na Benki ya CBA, iliyofanyika kwenye Kituo kikuu cha Mabasi, Mbagala Rangi Tatu, jijini Dar es Salaam jana.
Mdau Pina Mshana alikuwa ni mmoja wa waliochangia damu katika zoezi hilo, ikiwa ni muendelezo wa maadhimisho ya siku ya Damu Duniani.
Wachangia damu wakiwa kwenye foleni.