Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani
(kushoto), Mkuu wa Wilaya ya Kongwa Bw. Deogratius Ndejembi (wa pili
kushoto), pamoja na viongozi wengine wa Serikali wakikagua barabara ya
Hogoro - Kongwa KM 14.57 kwa kiwango cha changarawe wilayani humo,
mkoani Dodoma jana.
Serikali imesisitiza nia yake ya kuhakikisha ujenzi wa barabara ya Mbande-
Kongwa yenye urefu wa KM 11.71 inayojengwa kwa kiwango cha lami
unakamilika kwa wakati.
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani
amesema hayo mkoani Dodoma jana, mara baada ya kukagua sehemu ya
mradi wa barabara ya Mbande-Kongwa- Mpwapwa yenye urefu wa KM
49.14 ambao ujenzi wake unaendelea na kumuagiza Kaimu Meneja Wa
Wakala wa Barabara nchini (TANROADS), mkoa wa Dodoma Eng. Salome
Kabunda kusimamia mradi huo kikamilifu.
"Tutahakikisha fedha za mradi huu zinapatikana kwa wakati ili mradi
ukamilike mapema ikiwa ni mkakati wa kuifungua wilaya hii na kuhuisha
fursa za kimaendeleo kwa wananchi wa Wilaya ya Kongwa na Mpwapwa",
amesema Eng. Ngonyani.
Ameongeza kuwa kukamilika kwa mradi huo kutafungua fursa za
uwezekezaji katika maeneo hayo ikiwemo kurahisisha huduma za
usafirishaji wa mazao kwa Wilaya hizo mkoani humo.
Naye, Kaimu Meneja wa TANROADS, mkoa wa Dodoma Eng. Kabunda,
amemhakikishia Naibu Waziri kuwa watamsimamia Mkandarasi
anayejenga barabara hiyo kwa karibu ili ubora wa barabara hiyo uendane
na thamani ya fedha.
Aidha, Eng. Kabunda amewataka wananchi wa Wilaya ya Kongwa
kushirikiana na mkarandarasi ili kuwezesha ujenzi huo kwenda kwa
haraka.
Mkuu wa Wilaya ya Kongwa Bw. Deogratius Ndejembi ameishukuru
Serikali kwa kuanza ujenzi wa barabara hiyo kwani utachochea maendeleo
wilayani humo.
Takribani shilingi Bilioni 7.5 zinatarajiwa kutumika katika sehemu ya
kwanza ya mradi huo wa Mbande-Kongwa ambapo KM 5 zitajengwa na
zinatarajiwa kumalizika ndani ya miezi nane.
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani (kushoto), akizungumza na Mkuu wa Wilaya ya Kongwa Bw. Deogratius Ndejembi (kulia), wakati alipokuwa akikagua mradi wa ujenzi wa barabara ya Mbande - Kongwa KM 11.71 inayojengwa kwa kiwango cha lami, mkoani Dodoma jana.
Mkuu wa Wilaya ya Kongwa Bw. Deogratius Ndejembi (kulia), akifafanua jambo kwa Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani (kushoto), mara baada ya kukagua mradi wa ujenzi wa barabara ya Mbande - Kongwa KM 11.71 inayojengwa kwa kiwango cha lami, mkoani Dodoma jana.
Sehemu ya barabara ya Mbande - Kongwa yenye urefu wa KM 11.71 inayojengwa kwa kiwango cha lami, mkoani Dodoma jana.
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani (kulia), akitoa maelekezo kwa Kaimu Meneja wa Wakala wa Barabara nchini (TANROADS), Mkoa wa Dodoma Eng. Salome Kabunda (kushoto), wakati alipokuwa akikagua mradi wa ujenzi wa barabara ya Mbande - Kongwa KM 11.71 inayojengwa kwa kiwango cha lami, mkoani Dodoma jana.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...