Exim Bank Tanzania imetambuliwa kama Benki bora ya mwaka katika wateja binafsi na biashara ndogondogo na saizi ya kati, yaani ‘Retail banking’ katika tuzo za Banker za Afrika Mashariki zilizofanyika Nairobi, Kenya. 

Tuzo za Banker za Afrika Mashariki zimedhamiria kuhamasisha ubora kwenye sekta ya fedha katika kanda ya Afrika Mashariki. Kupitia kura 77,000 zilizopigwa na jamii ya sekta ya fedha katika kanda hii benki ya Exim ilichaguliwa kama mshindi wa mwaka huu katika wateja binafsi na biashara ndogo - Retail. 

Akiongea kwa niaba ya benki hiyo, Mkuu wa kitengo cha fedha Selemani Ponda alisema, “Tunajivunia sana na kushukuru kwa tuzo hii. Tumefanya kazi kubwa kwa muda mrefu kujenga msingi wa kuendeleza operesheni zetu za baadae. Matokeo yanajionyesha, katika miaka ya karibuni amana kutoka kwa wateja wetu imeongezeka na wateja pia wameongezeka. Vilevile faida baada ya kodi imeendelea kukua hadi kufikia kiasi cha shilingi bilioni 72 kwa mwaka 2016.” 

Ponda ambaye alihudhuria hafla ya tuzo hizo alitoa pongezi kwa waandaaji kwa kuandaa tukio lenye mafanikio kwa miaka mine mfululizo. Hadi sasa tuzo hizo zimevutia ushiriki wa wanataaluma wengi zaidi katika sekta ya benki katika kanda hii. Zaidi ya hapo aliongeza kuwa washirika muhimu kama vile kampuni za teknolojia ambazo husaidia kubadilisha sekta hii pia zilitambuliwa kwa mchango wao. 

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...