Kufuatia michuano ya mpira wa kikapu iliyozinduliwa na makamu wa raisi Mhe. Samia Suluhu Hassan wiki zilizopita, ameonyesha kuunga mkono zoezi hilo la kuwasaka wawakilishi lililofanyika katika mikoa mbalimbali. Sprite inaendelea kuibua hisia zaidi ikizileta pamoja zile timu zilizofuzu katika ngazi ya kimkoa kwenye fainali. 

Michuano ya kinyang'anyiro hiko yalishaanza toka 12 na tayari baadhi ya timu zilishaanza kuchuana huku kila timu ikiwa na matumaini makubwa ya kuibuka bingwa wa kudunda kikapu kitaifa mwaka 2017.
Finali hizi zitaendelea kupigwa mkoani Mwanza ndani ya viwanja vya chuo cha Butimba hadi tarehe 14 huku timu zikicheza mfululizo kwa mtoano ambapo bingwa atapatikana. Maandalizi yakiwa yamepamba moto, timu nazo zinaendelea kujinoa huku wachezaji wakijigamba kuwa mafahali katika finali hizo. 

Mshikemshike huu umewazoa mashabiki mbalimbali wa mpira wa kikapu kutoka Mwanza na wengine kutoka mikoa ya jirani kuja kushuhudia. Finali hizi pia zinasindikizwa na burudani za kukata na shoka kutoka kwa wasanii mbalimbali wa muziki ambapo msanii Dogo Janja alitokelezea kuchangamsha mshabiki na pafomansi la kibabe.

Washiriki wengine wakiwemo wadau wakubwa wa mpira wa kikapu nchini, pia wamejitokeza kushuhudia nani ataibuka kinara.
Lengo kubwa hasa la mashindano haya ni kuibua vipaji vya vijana katika michezo hususani mpira wa kikapu hapa nchini kuanzaia ngazi za chini hadi kitaifa. Na itakuwa ni fursa nzuri kwa vijana kujumuika pamoja na kuleta hamasa kwa vijana wengine kushiriki katika mchezo huu na hatimaye kuibua wachezaji mabingwa kitaifa hata kimataifa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...