THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

GOR MAHIA MABINGWA WA SPORTPESA SUPER CUP 2017, WAWATANDIKA FC LEOPARDS BAO 3-0

 Mabingwa ma Mashindabo ya SportPesa Super Cup 2017, Timu ya Gor Mahia kutoka nchini Kenya wakishangilia ushindi wao na Kombe la Ubingwa huo, baada ya kuwatandika wapinzani wao FC Leopards Mabao 3-0 katika mchezo uliomalizika hivi punde katika Uwanja wa Uhuru, Jijini Dar es salaam.
 Mabingwa ma Mashindabo ya SportPesa Super Cup 2017, Timu ya Gor Mahia kutoka nchini Kenya wakishuhudia Nahodha wao akipokea mfano wa hundi yenye thamani ya Dola elfu 30, baada ya kutwaa Ubingwa wa Mashindano hayo kwa kuwatandika wapinzani wao FC Leopards Mabao 3-0 katika mchezo uliomalizika hivi punde katika Uwanja wa Uhuru, Jijini Dar es salaam. 

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.

Timu ya Gor Mahia ya Kenya imetwaa ubingwa wa kwanza wa mashindano ya SportPesa Super Cup baada ya kuwasambaratisha wapinzani wao, AFC Leopards kwa mabao 3-0 kwenye uwanja wa Uhuru.

Kwa ushindi huo, Gor Mahia imepata nafasi ya kupambana na timu maarufu ya Ligi Kuu ya Uingereza, Everton FC  Julai 13 kwenye uwanja wa Taifa jijini.

Kwa ushindi huo, Gor Mahia ilizawadiwa Sh milioni 62 za Tanzania huku AFC Leopards ikiambulia Shilingi Milioni 22 kwa kushika nafasi ya pili.

Mabao ya Timotho Otieno katika dakika ya 60, OliverMaloba katika dakika ya 76 na John Ndirangu katika muda wa nyongeza yalitosha kuinyamazisha AFC Leopards kwenye fainali hiyo iliyokuwa ya kusisimua.

Dalili za ushindi kwa Gor Mahia zilionekana tokea mwanzoni  mwa mchezo huo ambapo mshambuliaji wake hatari, Medie Kagere alikosa baola wazi baada ya pasi nzuri ya GeorgeOdhiambo.

Baada ya kosa kosa hiyo, AFC Leopards ilikuja juu na kukosa nafasi tatu za kufunga kupitia kwa Gilbert Fiamenyo, Allan Katerega na Mangoli Benard. Mshambuliaji hatari wa Gor Mahia,Medie Kagere aliibuka  kuwa mfungaji bora wa mashindano hayo kwa kufunga mabao manne.