Mkurugenzi
Mtendaji wa Halotel, Le Van Dai, Akizungumza na waandishi wa habari
wakati kampuni hiyo ilipokuwa ikitoa pongezi kwa serikali kwa kuanzisha
mfumo wa wawazi wa ulipaji kodi kwa njia ya kielektroniki, Kampuni hiyo
ni miongoni mwa makampuni matatu ya simu ya kwanza kujiunga na mfumo huo
ambao amefafanua kuwa unaweka uwazi katika biashara. Pamoja nae katika
picha ni Meneja Uhusiano wa Kampuniu hiyo Stela Pius na Meneja
Mawasiliano Hindu Kanyamala (Kushoto).
Meneja
Mawasiliano wa Halotel, Hindu Kanyamala akifafanua jambo kwa waandishi
wa habari, Wakati kampuni hiyo ilipofanya mkutano wa kuipongeza serikali
kwa kuanzisha mfumo wa ulipaji kodi kwa njia ya kielectroniki. Katikati
ni Mkurugenzi Mtenzaji wa Kampuni hiyo Le Van Dai na Meneja Uhusiano
Stella Pius.
Pamoja
na mambo mengine Mkurugenzi huyo amesema kampuni hiyo bado inatoa
kipaumbele kwa kutoa huduma bora kwa jamii ya Watanzania ikiwepo pamoja
na kuwezesha miundombinu ya mawasiliano kwa taasisi mbalimbali za
serikali pamoja na taasisi za kijamii, zikiwemo shule, hospitali, ofisi
za posta na halmashauri mbalimbali. Hivi karibuni kampuni hiyo
ilitangaza uwekezaji wa Zaidi ya bilioni 200 katika kuboresha ubora wa
mtandao huo, ikilenga kuongeza kasi ya intaneti na ubora wa huduma za
sauti.
Kampuni
ya mawasiliano ya simu ya Halotel, imeipongeza serikali kwa kuweka
mfumo wa kukusanya kodi kwa njia rahisi na yenye uwazi na kufafanua kuwa
wao wamekuwa kampuni ya kwanza kujiunga na kufurahia utaratibu huo kama
ilivyobainishwa na kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA),
Charles Kichere, kwani unawezesha kampuni kuwa wazi katika malipo yote
ya kodi na tozo wanazozifanya kwa wateja.
Akizungumza
na waandishi wa Habari, Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo bwana Le
Van Dai, amefafanua kuwa wao kama kampuni siku zote wamejiweka mbele
katika kuhakikisha wanatimiza matakwa ya serikali kwa kufuata taratibu
zote zinazowekwa na mamlaka husika.
“Tulipofahamishwa
kuhusu utaratibu huu wa ukusanyaji kodi tulifurahia sana kwa sababu
unaweka wazi maendeleo ya biashara na ukusanyaji wa mapato ya serikali,
sisi kama wawekezaji tunafurahia kuwa na njia bora za usimamizi wa
mapato ya serikali na kampuni husika kwani unatuwezesha sisi pia
kujipima kujua biashara kama ni nzuri au sivyo na kuangalia namna bora
ya kushauriana na mamlaka husika katika kufanikisha mazingira bora ya
kibiashara” Alisema Dai.
Aidha,
Mkurugenzi huyo pia aliwaeleza waandishi wa habari kuwa wanaendelea
kufurahia mafanikio ambayo kampuni hiyo imekuwa ikiyapata tangu
kuanzishwa kwake.
“Katika
taarifa ya robo ya kwanza ya mwaka huu 2017 iliyotolewa na Mamlaka ya
Mawasiliano Tanzania (TCRA) imeonesha namna ambavyo kampuni yetu
imeendelea kufanya vyema katika kipindi cha miezi mitatu iliyopita,”
"Kimsingi,
idadi ya wateja wa kampuni za simu ilipungua kutoka 40,173,783 kwa
Desemba mwaka jana na kufika39,856,212 kwa Machi mwaka huu. Hii ina
maana kuwa kuna baadhi ya mitandao ya simu ilipoteza wateja ila Halotel
tumeweza kuongeza wateja wapya wapatao 73,872. Hii ni ishara kuwa
Watanzania wanaridhika na huduma zetu. Tunawaahidi kuwa
hatutawaangusha," alisema,”
Alisema
Dai na kuongeza kuwa “hii ni dalili nzuri kwetu kibiashara.
Tunawashukuru Watanzania kwa kuendelea kutuamini na kuendelea kujiunga
na sisi, tunawaahidi kuendelea kuboresha huduma zetu na kuufanya Halotel
uendelee kuwa Mtandao chaguo namba moja kwao.” Alihitimisha Mkurugenzi
huyo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...