NA TIGANYA VINCENT,TABORA.

SERIKALI ya mkoa wa Tabora imesema haitasita kuchukua hatua za kisheria kwa mtu yoyote atakayebainika kuendesha vitendo vya uharibifu wa ardhioevu kwa kuendesha shughuli za kibinadamu kama kilimo, ufugaji mifugo, uchomaji mkaa na uchomaji moto hovyo kwenye vyanzo vya maji na hifadhi za misitu.

Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri mara baada ya kushiriki kampeni ya upandaji na umwagiliaji wa miti ambalo ziliendeshwa na vijana 600 wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Msange ambao wametekeleza agizo la Makamu wa Rais kwa vitendo .

Alisema kuwa viongozi wote wanatakiwa kushirikiana na wananchi katika kuwabaini wote wanaoendesha shughuli hizo ovu katika mistu mkoani hapo kwa kuwa wanahatarisha wakazi wa Tabora na mikoa jirani.

Mkuu huyo wa Mkoa aliwashukuru vijana hao wa JKT waliomba kushiriki katika zoezi la kupanda miti kabla ya kumaliza mafunzo yao Jumamosi ili iwe alama ya uwepo wao katika eneo hilo.

Alisema kuwa kitendo walichoufanyia vijana hao kimeonyesha jinsi walifundishwa vizuri juu ya kuwa wazalendo kwa Taifa lao na kitabaki katika kumbukumbu za Mkoa huo na majina yao yataandikwa.


Mkuu wa Mkoa wa Tabora Bw. Aggrey Mwanri akizungumza na waandishi wa habari jana kabla ya kuanza zoezi la kuondoa magugu katika miti iliyopandwa katika Manispaa ya Tabora juzi.
Mkuu wa Mkoa wa Tabora Bw. Aggrey Mwanri akishirikiana na askari wa Kujenga Taifa(JKT) Msange wanaohitimu mafunzo yao Jumamosi wakati wa zoezi la kuondoa magugu katika miti iliyopandwa katika Manispaa ya Tabora juzi.Picha na Tiganya Vincent-RS -Tabora

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...