THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

MWENYEKITI WA CHADEMA LINDI SULEIMAN MATHEW NA MWENZAKE WAACHIWA HURU BAADA YA KUSHINDA RUFAA ZAO

Mahakama Kuu Kanda ya Mtwara imewaachia huru Mwenyekiti wa CHADEMA Mkoa wa Lindi Suleiman Mathew  (pichani) na mwenzake Ismail Kupilila ambaye ni Katibu wa CHADEMA Tawi la Nyangamara.. 

Viongozi hawa walihukumiwa adhabu ya kifungo miezi nane jela bila faini na Mahakama ya Wilaya ya Lindi mnamo 18.01.2017 na kufanikiwa kutoka kwa dhamana baada ya kukata rufaa na kukata hati ya ya dharura kwa ajili ya dhamana. 

Wakati anasoma hukumu hiyo Jaji Lameck Mlacha alisema kwamba kosa la kusanyiko lisilo halali linatakiwa kufanywa na watu watatu au zaidi sio wawili. Akasema pia kwamba vifungo vyao vimefutwa. Wako huru kwa sababu hawana hatia. 

Viongozi hao wa Chadema walihukumiwa kifungo cha gerezani tangu Januari mwaka huu, kabla ya kukata rufaa kupinga hukumu ya kesi hiyo iliyofunguliwa februari 8, mwaka jana na kutoka kwa dhamana .

Machi 7 mwaka huu Wakili wa viongozi hao wa Chadema, Deusdedit Kamalamo alisema kuwa baada ya mahakama kuwahukumu wateja wake kwenda jela miezi minane na kutoa nafasi ya kukata rufaa, walikata rufaa na kukata hati ya dharura kwa ajili ya dhamana. 

Mahakama Kuu iliwaachia kwa dhamana Mwenyekiti wa Chadema Mkoa wa Lindi, Seleman Methew na Katibu wa Tawi wa kata ya Nyangamala, Ismail Kupilila waliokuwa wakitumikia kifungo cha miezi minane kwa kosa la kufanya mikutano bila kibali baada ya kuona kuna kesi ya kusikiliza. 

Kabla ya kutoa uamuzi wa kesi hiyo namba 1 ya mwaka 2017, Jaji Lameck Mlacha wa Mahakama Kuu, Kanda ya Mtwara, alisikiliza hoja za pande zote mbili katika shauri hilo na baadaye kuwaachia huru kwa kuwataka waweke dhamana ya sh. 2 milioni kwa kila mmoja.
Viongozi hao wa Chadema wamekuwa gerezani tangu Januari mwaka huu, kabla ya kukata rufaa kupinga hukumu ya kesi hiyo iliyofunguliwa februari 8, mwaka jana.