THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

IGP SIRRO AWAFARIJI WAFIWA KIBITI

 Mkuu wa Jeshi la polisi nchini IGP Simon Sirro akisalimiana na wananchi wa kijiji cha Mangwi, kata ya mchukwi wilayani kibiti jana alipokwenda kuwapa pole baada ya kutokea mauaji ya mwenyekiti wa kitongoji na afisa mtendaji wa kijiji. Picha na Hassan Mndeme-Jeshi la polisi.
Mkuu wa Jeshi la polisi nchini IGP Simon Sirro akizungumza na wananchi wa kijiji cha mangwi, kata ya mchukwi wilayani kibiti jana alipokwenda kuwapa pole baada ya kutokea mauaji ya mwenyekiti wa kitongoji na afisa mtendaji wa kijiji hicho. IGP Sirro alitumia fursa hiyo kuwataka wananchi kijijini hapo kutowafumbia macho wahalifu wanaotenda mauaji hayo na kuwataka kuwa na kushirikiana na jeshi la polisi kwa kutoa taarifa za wahalifu hao.  picha na hassan mndeme-jeshi la polisi.
 Mkuu wa Jeshi la polisi nchini IGP Simon Sirro akitoa rambirambi ya msiba kwa wananchi wa kijiji cha mangwi, kata ya mchukwi wilayani kibiti jana alipokwenda kuwapa pole baada ya kutokea mauaji ya Mwenyekiti wa kitongoji na Afisa Mtendaji wa kijiji hicho. picha na Hassan Mndeme-Jeshi la Polisi.
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro akikagua nyumba iliyochomwa moto na wahalifu waliofanya mauaji ya mwenyekiti wa kitongoji na afisa mtendaji wa kijiji cha mangwi, kata ya mchukwi wilayani kibiti jana alipokwenda kuwapa pole baada ya kutokea mauaji  hayo. picha na hassan mndeme-jeshi la polisi.Hoja moja imeshachangiwa mpaka sasa.

  1. maturamatara Anasema:

    Poleni sana Kibiti
    Hawa majangili uchwara inaonyesha si wakazi wa Kibiti au Pwani otherwise wasingetaka wapelekwe wanapoishi viongozi. Pili IGP kwa nini usiwatume vijana wako wakajifanye viongozi wa serikali ili muwakamate hawa majuha? as u can c tageti yao ni viongozi..... mwaga askari kanzu wakagombee uongozi. vitu vidogo kama hivi vikifanyiwa mzaha huwa vikubwa