Naibu Waziri wa Nchi ,Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa  (TAMISEMI)Mhe.Selemani Jafo amewataka vijana wa Taasisi ya Maendeleo ya Vijana Dodoma(DOYODO) kuongeza ubunifu ili waweze kuwa washindani katika soko la biashara kwa kutumia fursa ya  wahamiaji wanaokuja Dodoma.

Mhe.Jafo aliyazungumza hayo alipokuwa anakagua miradi mbalimbali ya taasisi hiyo mapema leo na kuwataka kuwekeza kwenye kilimo  kwa kuwa   wanafikilia kupata eneo lao wenyenye ni vyema  kupata hekari moja kwa ajili ya kilimo cha mboga mboga na matunda kwani kinalipa.

’’Kumekuwa na tabia ya vijana kuchagua kazi na baadhi yao kusubiri kupata ajira kutoka Serikalini lakini nyie mmetoa mfano badala ya kutegemea ajira, mmejiajiri na ntahakikisha baadhi ya wabunge wanakuwa wa kwanza kuja kununua matofali hasa kwa wale wanaojenga Dodoma ’’

“Nitaongea na Mkurugenzi wa Manispaa ya Dodoma ili mpatiwe milioni moja kutoka mfuko wa 5% ya makusanyo ya Manispaa ya Mapato ya vijana na milioni kumi kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu na mimi nachangia  kwa kununua matofali mia tano “Mhe.Jafo aliahidi.

Naye Afisa Mipango na Muhasibu wa DOYODO Elias Mbogo amesema taasisi inajipatia kipato chake kupitia vyanzo mbalimbali ikiwemo ada ya uanachama,tozo,miradi yao na misaada kutoka kwa wadau wa Taasisi. 

Taasisi ya DOYODO imesajiliwa kisheria mwaka 2002 na kuanza kufanya shughuli zake rasmi toka 2015 na miradi waliyonayo ni mradi wa matofali,tuition(elimu),ufundi chelehani na kukodisha ukumbi kwa ajili ya semina na sherehe mbalimbali.
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe. Selemani Jafo akizungumza na waandishi wa habari akiwataka vijana wa taasisi ya DOYODO kuwa mfano wa kuigwa Dodoma na nchi nzima katika kampeni yao ya kujiajiri wenyewe.
 Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe.Selemani Jafo akiwasha mtambo wa kufyatulia matofali.
 Naibu Waziri wa  Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe.Selemani Jafo akizungumza na Wanafunzi waliokuwa wanafundishwa masomo ya ziada(tution) katika ofisi ya DOYODO.


 Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe. Selemani Jafo akiwa katika picha ya pamoja na vijana wa taasisi ya DOYODO na Afisa Vijana kutoka Manispaa ya Dodoma alipokuwa anakagua miradi mbalimbali mapema leo ofisini kwao mjini Dodoma.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...