NAIBU Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo amewataka Wakuu wa wilaya kuacha historia katika utendaji wao (legacy) kwenye maeneo wanayoongoza.

Naibu Waziri Jafo aliyasema hayo mjini Morogoro alipokuwa akifungua semina kwa Wakuu wa wilaya ya kuwajengea uwezo katika usimamizi wa Miradi ya Maendeleo katika sekta ya Kilimo awamu ya pili(ASDPII) itakayotekelezwa kwa kipindi cha mwaka 2017/2018 hadi 2027/2028.

Akifungua semina hiyo, Jafo amewataka wakuu hao washindane katika kufanikisha Mipango ya maendeleo ya serikali ili kuinua uchumi wa mtu mmoja mmoja na Taifa kwa ujumla. Kadhalika, amewataka wakurugenzi wa Halmashauri kuwapa taarifa za fedha za maendeleo ya miradi hiyo wakati wa utekelezaji ili wakuu hao wa wilaya waweze kufuatilia mwenendo wa utekelezaji wa Miradi hiyo.

Jafo amesisitiza kwamba katika kipindi cha hichi ambacho kuelekea uchumi wa viwanda hapa nchini sekta ya kilimo ndio inategemewa kuzalisha malighafi za viwandani. Aidha amewataka wakuu hao wa wilaya kusimamia vyema sekta ya Kilimo ili Tanzania licha ya kutegemea mazao ya biashara kwa fedha za kigeni sasa Tanzania ijielekeze pia kuzalisha mazao mengi ya chakula.

Amesema ukifanyika uzalishaji wa mazao ya chakula na ziada ya mazao hayo kuyauza nje ya nchi yataongeza fedha za kigeni nchini. “Tuna uwezo wa kufanya hivyo kutokana na uwepo wa ardhi ya kutosha yenye rutuba na vyanzo vingi vya Maji,”amesema Jafo

Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tamisemi selemani Jafo akiwa katika picha ya pamoja na wakuu wa wilaya.

Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tamisemi selemani Jafo akiwa kwenye picha ya pamoja na wadau wa maendeleo pamoja waratibu wa ASDP II wa Ofisi ya Rais TAMISEMI na Ofisi ya Kilimo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...