THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

KAMPUNI YA MAZIWA YA ASAS DAIRIES LTD YANYWESHA MAZIWA WANAFUNZI WA SHULE ZA MSINGI MANISPAA YA IRINGA


WAKATI leo ni siku ya unywaji maziwa duniani kampuni ya maziwa ya Asas Dairies Limited imenywesha maziwa wanafunzi zaidi ya 4000 wa shule mbali mbali za Manispaa ya Iringa .

Shule hizo za msingi zilizopo kanda ya Ruaha ambazo zimeanza kunufaika na unywaji maziwa ,huku walimu wao wakidai baadhi ya wanafunzi wa shule hizo wamekuwa na matokeo mabaya katika mitihani kutokana na unywaji wa pombe ya kienyeji aina ya ulanzi .

Meneja wa miradi wa kampuni ya Asas Dairies Ltd Hassan Swedi alisema kuwa maadhimisha ya mwaka huu yamelenga zaidi vijana hasa wanafunzi wa shule za msingi mjini Iringa na ndio sababu kampuni yake imelazimika kutoa msaada wa maziwa na majaketi kwa wanafunzi wanaotoka katika familia duni .

Alisema kuwa kampuni hiyo inaamini kuwa iwapo shule zitaweka utaratibu wa kutoa maziwa kwa wanafunzi afya za wanafunzi hao zitakuwa bora na kiwango cha elimu kinaweza kuongezeka zaidi mashuleni.

Mbali ya unywaji wa maziwa kuhamasishwa zaidi mashuleni bado viongozi wa serikali wanapaswa kuanza kuhamasha unywaji wa maziwa katika ofisi hizo za umma badala ya kutumia maziwa kutoka nje ya nchi .
Alisema kuwa kampuni ya Asas Dairies

Ltd imeendelea kuunga mkono mpango wa lishe mashuleni kama njia ya kuboresha afya na uwezo wa wanafunzi kufanya vizuri kwenye masomo Iringa unazalisha maziwa zaidi ya lita milioni 14 kwa mwaka ila bado kiwanda cha Asas kinasindika lita 400,000 pekee kwa siku .

Meneja miradi wa kampuni ya maziwa ya Asas Dairies Ltd Hassan Swedi akimpa maziwa mlemavu 
leo siku ya unywaji maziwa duniani

wafanyakazi wa kampuni ya Asas wakigawa maziwa kwa wanafunzi leo siku ya unywaji maziwa duniani .