THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

KATIBU MKUU WIZARA YA ARDHI DKT. KAYANDABILA AAGWA RASMI NA WATUMISHI WA WIZARA HIYO

Aliyekuwa Katibu Mkuu, Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi; Dkt. Yamungu Kayandabila amesisitiza utumishi bora unaozingatia Miongozo na Sheria.
Dkt. Kayandabila aliyeteuliwa hivi karibuni na Mhe. Rais, Dkt. John Pombe Magufuli kuwa Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), akiwaaga Watumishi wa Wizara alihimiza utendaji bora kazini katika kutoa huduma kwa Wananchi na kusihi Watumishi kuendelea na kasi hiyo.
Aidha, aliwashukuru Watumishi wa Wizara ya Ardhi kwa ushirikiano wao walioonyesha kwake ambao umesababisha kudhihirisha matukio chanya kwa Wizara. Alisema; “ Tukumbuke kuwa sisi ni Watumishi wa Umma, tuendelee kufanya kazi kwa bidii kwa kuwahudumia Wananchi kwa bidii”.
Awali akizungumza kwa niaba ya Watumishi wa Wizara; Afisa Mipango Miji, Baltazar Sumari alisema; “ Tunakushukuru Katibu Mkuu kwa jinsi ulivyotuwezesha kufanya kazi kwa umoja na nidhamu, Mungu akuwezeshe uweze kuendelea kudumisha utendaji wako wa kazi Benki Kuu kama jinsi ulivyofanya Wizarani hapa na tutaendelea kuhitaji ushauri wako”.
Naye muwakilishi wa Taasisi za Wizara; Msajili wa Bodi ya Usajili wa Wataalamu wa Mipangomiji (TPRB);  Helena Mtutwa alisema kuwa Dkt. Kayandabila ana karama ya kipekee ambayo imemuwezesha kuongoza vyema kwa kuweza kuonyesha njia bora katika utendaji kazi na kuonya kwa hekima.  
Dkt. Kayandabila anakwenda kutumika katika Benki Kuu ya Tanzania kama Naibu Gavana anayeshughulikia Uchumi na Fedha (Economic and Financial Policies – EFP), akiwa na Naibu Gavana mwenza aliyeteuliwa naye kwa kipindi kimoja; Dkt. Bernard Yohana Kibese atakayehusika katika eneo la Uthabiti na Usimamizi wa Sekta ya Fedha (Financil Stability and Deepening – FSD).
Na kitengo cha Mawasiliano Serikalini – 
Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi
 Aliyekuwa Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt. Yamungu Kayandabila akizungumza na watumishi alipokua akiwaaga. Dkt. Kayandabila ameteuliwa na Mhe. Rais kuwa Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania. (BoT).
 Aliyekuwa Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt. Yamungu Kayandabila akipokea zawadi, ikiwa ni ishara ya pongezi kwa uteuzi wake mpya alioupata. Anayemkabidhi zawadi hiyo kwa niaba ya watumishi wa wizara ni Naibu Katibu Mkuu, Dkt Mosses Kusiluka.
Watumishi wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi katika picha ya pamoja na aliyekuwa Katibu Mkuu wa wizara hiyo; Dkt. Yamungu Kayandabila mara baada ya kuwaaga.