THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

Kesi ya lugha ya uchochezi dhidi ya Tundu Lissu yaendelea kuungruma mahakamani.

Na Karama Kenyunko, blogu ya jamii .

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imeelezwa kuwa, Mbunge wa Singida Mashariki kupitia tiketi ya Chadema, Tundu Lissu alikamatwa baada kutolewa kwa amri ya kufanyika hivyo kutoka kwa Mkuu wa Upelelezi Kanda Maalum (ZCO).  

MKUU wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai wa Wilaya (OCCID), Yustino Mgonja ameeleza hayo leo mbele ya Hakimu MKazi Godfrey Mwambapa wakati akitoa ushahidi wake kama shahidi wa nne katika kesi ya kutumia lugha ya uchochezi inayomkabili Lissu ilipokuja kusikilizwa.

Akiongozwa na Wakili Mwandamizi wa Serikali, Mutalemwa Kishenyi, Mgonja amedai kuwa Juni 28, mwaka jana, ZCO Wambura alimpa maelekezo ya kumkamata Lissu kwa kosa la kutoa lugha za uchochezi katika Viwanja vya mahakama hiyo.
Amedai, Juni 29 mwaka jana, majira ya mchana alienda nyumbani kwa Lissu maeneo ya Tegeta wilayani Kinondoni ambapo alimkamata na kumfikisha katika Ofisi za ZCO na kumkabidhi.
Alidai kuwa, alipewa amri na ZCO kumkamata Lissu  na alifanya hivyo licha ya kuwa hakuwa na hati ya ukamataji kwa kuwa mamlaka yalikuwa yanamruhusu kufanya hivyo na kuwa mtu yoyote akifanya makosa ya jinai unaruhusiwa kukamata bila kuwa na hati. 
Aliongeza kuwa, kumpinga Rais anapokosea sio kosa na kwamba tafsiri ya maneno aliyoyatoa ndio yamesababisha kukamatwa na kushitakiwa kwa kutumia lugha za kichochezi.
Lissu anadaiwa kuwa Juni 28, mwaka huu, akiwa katika viwanja vya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, alitoa kauli za uchochezi kuwa, “Mamlaka ya Serikali mbovu ni ya kidikteta uchwara inahitaji kupingwa na kila Mtanzania kwa nguvu zote, “huyu diktekta uchwara lazima apingwe kila sehemu”. Kama uongozi utafanywa na utawala wa kijinga nchi inaingia ndani ya giza nene.’’