THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

Kesi ya meno ya Tembo ya Milioni 13 dhidi ya Raia wa China na Watanzania sasa kusikilizwa kwa usiri

Na Karama Kenyunko

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imeridhia ombi la upande wa mashtaka la kutaka ushahidi utakaotolewa na askari polisi kutoka Makao Makuu ya Upelelezi wa Makosa ya Jinai Kitengo cha kupambana na Ujangili,D 7847 Sajenti Beatus usikilizwe kwa usiri.

Ushahidi huo ni katika kesi ya  uhujumu uchumi kwa kujihusisha na Meno ya Tembo ya bilioni 13 inayomkabili  raia wa China anayedaiwa kuwa Malkia wa Pembe za Ndovu, Yang Feng Glan (66)na watanzania wawili.

Mapema wakili wa Serikali Paul Kadushi, aliiomba Mahakama hiyo  ushahidi wa askari huyo ambaye awali alikwishaanza kutoa ushahidi wake kwa uwazi, usikilizwe kwa usiri kwa sababu unahusisha masuala ya amani ndani ya nchi.

Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi alikubaliana na ombi hilo la upande wa mashtaka kusikilizwa kwa usiri.

Hata hivyo, mmoja wa mawakili wa utetezi, wa Masumbuko Lamwai alilipinga hilo na kudai kuwa hakuna mahusiano juu ya Pembe za Ndovu na amani ya nchi.

Alidai kuwa, upande wa mashtaka hawakueleza ni kwa namna gani ushahidi wa Pembe za Ndovu utaingiliana na amani na utulivu katika nchi hii.

Aliongeza kuwa, mtu yoyote anayetuhumiwa kutenda kosa ni haki yake kikatiba,kesi isikilizwe hadharani ili kuhakikisha Haki ionekane imetendeka na umma ujue.

 Aliongeza kuwa kufanya hivyo kunaleta uwezekano wa mtu kuleta ushahidi wa kubambika.

Alibainisha kuwa upande wa mashtaka haujaweza kutoa sababu kwa nini ushahidi wa shahidi huyo uendelee kusikilizwa kwa usiri wakati ndugu wana Haki ya kujua hii kesi inaendeleaje.

" Kesi imekuwa kijamii mno, halafu isikilizwe kwa usiri kama mahakama ya kijeshi siyo Haki, mteja wangu amepewa Umalkia wa Pembe za Ndovu huo umalkia uthibitishwe hadharani siyo kisiri siri tunaomba hilo ombi likataliwe." Aliomba Lamwai.