Na Karama Kenyunko, Globu ya jamii.

Othman Mzange maarufu kama Julius Lyimo ama Anthony Mathew Hakalu amepandishwa katika kizimba cha Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu akikabiliwa na mashtaka matano likiwemo la kumdanganya mchunguzi wa Takukuru na kujipatia milioni 105 kwa njia ya udanganyifu.

Mshtakiwa amesomewa mashtaka yake na Wakili wa Serikali Mwandamizi Vitals Peter mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu,Godfrey Mwambapa.

Katika shtaka la kwanza imedaiwa kuwa,  tarehe  tofauti tofauti 2011, katika ofisi ya Takukuru Dar es salaam, wakiwa kwenye uchunguzi wa kesi namba PCCB/HQ/ENQ/07/2016 kwa mshtakiwa alimdanganya afisa uchunguzi wa Takukuru kwa kujitambulisha kwake kuwa yeye ni Antony Mathew Hakalu kwa nia ya kuficha uhalisia wake.

Imedaiwa kuwa, January 28,2009 katika Manispaa ya Kinondoni mshtakiwa kwa makusudi, aliwasilisha katika ofisi ya ardhi Manispaa ya Kinondoni barua yenye namba TIB/ORG/59/1/A ya Januari 2009 kwa madhumuni ya kuonyesha benki ya TIB ikiwa  kama mfilisi wa Tanzania Housing Bank(THB) imeuza ploti namba 596 iliyopo Mikocheni kwa Julius Lyimo.

Aidha, mshtakiwa anadaiwa siku na mahali hapo aliandika barua ya uongo kwa afisa ardhi wa Manispaa ya Kinondoni kwa madhumuni ya kuonesha Benki ya TIB ikiwa kama mfilisi wa THB imeuza ploti namba 596 iliyopo Mikocheni kwa Julius Lyimo.

Mshtakiwa huyo pia anadaiwa kuwasilisha hati ya kiapo ya uongo katika Manispaa hiyo kwa madhumuni ya kuonesha kiapo hicho kimeapwa na Hakimu wa Mahakama ya Mwanzo Kinondoni, M. Mriam ambayo ilikuwa ikisema Julius Lyimo amezaliwa mwaka 1952.

Mshtakiwa huyo kwa njia ya udanganyifu, alijipatia milioni 105 kutoka kwa Josia William Masonu kwa kujifanya yeye ni mmiliki wa hizo ploti namba 596 yenye hati namba 82320 L.O namba 350982 KMC/LD/5487 iliyopo Mikocheni Manispaa ya Kinondoni na kwamba alikuwa na uwezo wa kuiuza  kwa Josia, huku akijua kuwa siyo kweli.

Mshtakiwa amekana mashtaka hayo na amerudishwa rumande kwa kushindwa kutimiza masharti ya dhamana. Kwa mujibu wa mwendesha mashtaka, upelelezi umekamilika na kesi hiyo itatajwa Julai 4, mwaka huu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...