THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

KUELEKEA SIKU YA MAZINGIRA DUNIANI.

Usafi wa kila mwisho wa mwezi waimarisha mazingira nchini

KILA ifikapo Juni 5 kila mwaka, zaidi ya nchi 100 zinaadhimisha Siku ya Mazingira Duniani. Jovina Bujulu wa Idara ya Habari (MAELEZO) anaelezea umuhimu wa siku hii ambayo hapa nchini itaadhimishwa tarehe 3 na 4 mkoani Mara katika kijiji cha Butiama. 

Madhumuni makubwa ya maadhimisho haya ni kuhamasisha jamii duniani kote kuelewa masuala yanayohusu mazingira na pia kuhamasisha watu kulinda na kuhifadhi mazingira. Aidha, ni siku ambayo jamii inatakiwa kutambua umuhimu wa kulinda na kuhifaddhi mazingira kwa ustawi na maendeleo ya nchi.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Ofisi ya Rais, Muungano na Mazingira, maadhimisho hayo mwaka huu yatafanyika kijijini Butiama ili kumuenzi Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere na kukumbuka mchango wake mkubwa katika masuala ya mazingira.

Wakati wa maadhimsho hayo shughuli mbalimbali zitafanyika zikiwemo kupanda miti, kuendesha mijadala mbalimbali na kongamano la viongozi kuhusu mazingira na pia kufanya maonyesho ya shughuli za mazingira.

Mgeni rasmi katika maadhimisho hayo ambayo Kauli Mbiu ya mwaka huu niHifadhi ya Mazingira: Muhimili kwa Tanzania ya Viwanda atakuwa Makamu wa Rais, Mh. Samia Suluhu Hassan. Kaulimbiu hii inahamasisha Utunzaji wa mazingira wakati tukielekea uchumi wa viwanda.

Tarehe 9 Desemba mwaka jana, Rais wa Awamu ya Tano Dkt. John Pombe Magufuli aliamuru kusitisha maadhimisho ya Kitaifa ya Siku ya Uhuru wa Tanganyika na badala yake siku hiyo iadhimishwe kwa kufanya usafi wa mazingira nchini kote.