Afisa Maliasili Mkoa wa Mbeya Ndugu, Joseph Butuyuyu akizungumza na Globu ya Jamii alipokuwa  juu ya Maadhimisho ya kilele cha mazingira duniani yanayo tarajia kufanyika Juni 5, mwaka huu ambapo kimataifa yatafanyika Nchini Canada, na Kitaifa yatafanyika Mkoani Mara na Kwa Mkoa wa Mbeya yanatarajiwa kufanyika wilayani Mbarali katika eneo la Mabadaga siku hiyo ya Jumatatu na mgeni Rasmi kwa mkoa wa Mbeya Atakuwa ni mkuu wa mkoa wa mbeya Mh.Amos G. Makalla na watu wote mnakaribishwa.
Ndugu, Joseph Butuyuyu Pia aliongeza kwa kuwataka wananchi wa mkoa wa mbeya kutunza na kuthamini mazingira yanayo wazunguka ili kupendezesha na kuyatunza vizuri mazingira ya mkoa wa mbeya na kuwataka wananchi kuchungamkia fursa ya kutembelea vivutio mbalimbali ikiwemo mbuga za wanyama bira kulipa kiingilio chochote kwa siku tatu mfululizo kuanzia siku ya Tarehe 2, mpaka Tarehe 4, ya mwezi huu.

Kauli mbiu ya Maadhimisho ya Mazingira Duniani kwa mwaka huu ni   (Mausiano endelevu kati ya Binadamu na Mazingi) hiyo ikiwa ni kimataifa na kitaifa ni.. Hifadhi ya Mazingira ni Muhimili kwa Tanzania ya Viwanda.
NA MR.PENGO MBEYA.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...