Mabenki yameombwa kuwa tayari kukopesha mnyonyororo mzima wa sekta ya kilimo na mifugo hili kuunga mkono juhudi za Serikali za kuinua ukuaji wa uchumi na kupunguza umaskini nchini.

Hayo yamesemwa na Mwakilishi wa Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB), Bw. Augustino Chacha wakati akifungua mafunzo ya awamu ya pili yanayohusiana na Kanuni za Ukopeshaji katika Kilimo yanayoendeshwa kwa ushirikiano wa pamoja kati ya TADB, Benki ya Taifa ya Kilimo na Maendeleo Vijijini India (NABAD) na Programu ya Miundombinu ya Masoko, Uongezaji Thamani Mazao na Huduma za Kifedha Vijijini (MIVARF).

Bw. Chacha amesema kuwa mabenki na taasisi za kifedha nchini hazina budi kuwekeza mtaji wa kutosha ili kuweza kukopesha sekta ya kilimo ambayo ni uti wa mgongo wa Tanzania na ambayo inaajiri zaidi ya asilimia 75 ya watu wenye uwezo wa kufanya kazi nchini na pia kutoa kiasi cha zaidi ya asilimia 65 cha mali ghafi kwa ajili ya viwanda vya nchi.

Ameongeza kuwa kuanzinshwa kwa TADB kunalenga kuwezesha mabenki ya biashara kupata fedha zenye masharti nafuu na endelevu ili ziweze kukopesha sekta ya kilimo ili kuchagiza na kusaidia Mapinduzi ya Kilimo kutoka kilimo cha kujikimu kwenda cha kibiashara ili kuchangia kwenye ukuaji wa uchumi na kupunguza umaskini.
Mwakilishi wa Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB), Bw. Augustino Chacha akizungumza wakati akifungua mafunzo ya awamu ya pili yanayohusiana na Kanuni za Ukopeshaji katika Kilimo. Mafunzo hayo ya awamu ya pili yatafanyika kwa siku sita yanaendeshwa kwa pamoja kati ya TADB, NABAD na MIVARF.
Mkuu wa Idara ya Majanga na Vihatarishi, Bw. Adam Kamanda (kulia) akizungumza nafasi ya TADB katika kuwezesha Mabenki na Taasisi za Fedha nchini kuweza kukopesha wakulima.
Meneja Msaidizi wa Mafunzo kutoka NABAD, Dkt. R.S. Reddy akifundisha namna ya kufanyia uchambuzi miradi ya kilimo ili kuongeza tija kwenye utoaji wa mikopo kwenye sekta hiyo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...