Askari wa Usalama Barabarani akichukua maelezo ya gari Noah yenye namba za usajili T338 BVU iliopata ajali mapema jana,njia panda Goba,Mbezi Beach jijini Dar.Baadhi ya Mashuhuda wa tukio hilo walieleza kuwa chanzo cha ajali hiyo ni mwendo kasi wa gari dogo (daladala pichani chini yenye namba za usajili T912 CVY),iliyokuwa imebeba abiria ikitokea Goba kwenda Mwenge,na hivyo gari hiyo kukosa mwelekeo kufuatia kona kali iliyopo eneo hilo,Katika ajali hiyo hakuna aliyepoteza maisha.

Mashuhuda hao pia wakatoa wito kwa baadhi ya Madereva kuwa makini,kufuata sheria na kuzingatia alama za barabarani,kwani kwa kufanya hivyo ajali nyingi zitapungua kutokea. 
  Daladala yenye namba za usajili T912 CVY ikiwa imeacha barabara na kuvamia mtaro kufuatia gari hiyo kupoteza uelekeo kwa kile lichodaiwa na Mashuhuda kuwa ni mwendo kasi na kutaka kugongana uso kwa uso na gari nyingine aina ya Noah (pichani juu),sehemu yenye kona kali.
Baadhi ya watu wakishuhudia ajali ya gari aina  daladala pichani yenye namba za usajili T912 CVY,ikiwa imeacha njia na kuvamia mtaro,kama ionekavyo pichani.katika ajali hiyo hakuna aliyepoteza Maisha

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...