Serikali imesema ujenzi wa maegesho ya kivuko Mkoani Lindi utakamilika mwezi Novemba mwaka huu ili kurahisisha usafirishaji wa abiria na mizigo kwa wakazi wa eneo la Kitunda Mkoani Lindi.

Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa alipokagua maendeleo ya ujenzi wa maegesho hayo na kusema ujenzi huo umegharimu kiasi cha Tsh, bilioni 1.8 ambazo zitahusisha maegesho ya Kivuko na kujenga barabara ya kiwango cha lami mita 150 upande wa Kitunda Mkoani Lindi.

‘Tuliahidi na sasa tunatekeleza, nimefurahi kuona ujenzi unaendelea vizuri na ninawahakikishia mwezi Novemba tutakuja kuzindua kivuko’ alisema WazirI Profesa Mbarawa.

Aidha,Waziri Mbarawa amemtaka Mkandarasi anaejenga magesho hayo kuzingatia thamani ya fedha wakati wa ujenzi wake ili mradi huo uweze kudumu kwa muda mrefu.

‘hakikisha unajenga maegesho haya kwa kuzingatia viwango tulivyokubaliana, hatutaki kuona kasoro mara tu baada ya mwezi mmoja, hizi ni fedha za walipa kodi na tunategemea miundombinu hii ikae muda mrefu’ alisisitiza Waziri Prof. MBARAWA.

Kwa upande wake Msimamizi wa Mradi huo, Meneja wa Wakala wa Barabara nchini (Tanroads), mkoa wa Lindi, Eng. Issack Mwanawima amemuhakikishia Waziri Profesa Mbarawa kuwa watasimamia mradi kwa kuzingatia viwango katika ujenzi huo na kuhakikisha unakamilika kama mkataba unavyosema.
Meneja wa Wakala wa Barabara Nchini (TANROADS). Mkoa wa Lindi,Eng. Issack Mwanawima (mwenye koti la draft), akimweleza Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa (kushoto), hatua iliyofikiwa katika ujenzi wa maegesho hayo, Mkoani humo, wakati Waziri huyo alipotembelea mradi huo hivi karibuni.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa (kulia), akiangalia ujenzi wa wa maegesho ya kivuko unaojengwa katika mkoa wa Lindi alipotembelea mradi huo hivi karibuni. Mradi huo utahusisha maegesho ya kivuko na ujenzi wa mita 150 za barabara ya lami upande wa Kitunda.
Tinga Tinga likiendelea na ujenzi wa maegesho ya kivuko Mkoani lindi. Ujenzi wa maegesho hayo unatarajiwa kukamilika mwezi Novemba mwaka huu.
Meneja wa Bandari ya Mtwara, Eng. Juma Kijavara (katikati), akimuonesha Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa (kushoto), eneo la gati ya Lindi ambalo litatakiwa kuchimbwa ili kuongeza kina cha gati hilo, alipotembelea gati hiyo hivi karibuni.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...