Mkurugenzi Mkuu wa WCF, Bw. Masha Mshomba, akimkabidhi Dkt.Kezia, cheti cha ushiriki wa mafunzo ya tathmini ya ajali na majeraha kwa mfanyakazi aliyeumia wakati akitekeleza majukumu yake mahala pa kazi, wakati wa kilele cha mafunzo ya siku tano kwa madaktari kutoka hospitali za umma na binafsi za jijini Dar es Salaam. Jumla ya madaktari 70 kutoka hospitali 35 walishiriki.
NA K-VIS BLOG/Khalfan Said

MAFUNZO ya siku tano kwa madaktari yaliyoandaliwa na Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, (WCF), ili kuwajengea uelewa wa namna ya kufanya tathmini ya ugonjwa na ajali kwa mfanyakazi aliyepata madhara mahala pa kazi yamemalizika kwa washiriki kutunukiwwa vyeti.

Mafunzo hayo yaliyofunhga na Mkurugenzi Mkuu wa WCF, Bw. Masha Mshomba makao makuu ya Mfuko huo, jingo la GEPF barabara ya Bagamoyo jijini Dar es Salaam, Juni 23, 2017, yaliwaleta pamoja madaktari 70 kutoka hospitali mbalimbali za umma na binafsi jijini Dar es Salaam.

Mafunzo hayo yaliyogusa maeneo mbalimbali pia yaliwawezesha madaktari hao kujifunza Muongozo mpya unaohusu namna ya kufanya tahmini kabla ya kumlipa fidia stahiki Mfanyakazi aliepata madhara mahala pa kazi.

Akizungumza kwenye ufungaji wa mafunzo hayo, Mkurugenzi Mkuu wa WCF, Bw Masha Mshomba, alisema kuwa ni iani ya Mfuko kuwa Madaktari hao wamefaifika na mafunzo hayo na yatawezesha ufanisi katika kjutoa huduma hizo kwa wafanyakazi waliopata magonjwa au kuumia wakati wakiwa kazini.
Dkt.Benjamin Najimu Mohammed, akizungumz kwa niaba ya madaktari wenzake. "Nia ya mafunzo haya ni kwenda kuwasaidia watanzania wenzetu kwa niaba ya wenzangu napenda kuushukuru Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, kwa kutambua umuhimu wa ushiriki wetu katika mafunzo haya ili hatimaye kuwasaidia walengwa ambao ni watanzania wenetu." Alisema Dkt. Mohammed kutoka hospitali ya Kairuki ya Mikocheni jijini Dar es Salaam.

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...