Na
Mary Gwera, Mahakama, Iringa
Mahakama ya Hakimu Mkazi
Iringa imefanikiwa kuondosha Mashauri/kesi kwa zaidi ya asilimia tisini (90) na
kuifanya Mahakama hiyo kuendana na azma ya Mahakama ya Tanzania ya kutoa haki
kwa wakati ili kuondokana na mlundikano wa mashauri katika Mahakama zake
nchini.
Akizungumza ofisini
kwake katika mahojiano maalum na Mwandishi wa taarifa hii aliyepo Kanda ya
Iringa, mapema Juni 6, Hakimu Mkazi Mfawidhi, Mahakama ya Hakimu Mkazi-Iringa,
Mhe. David Ngunyale alisema hali ya uondoshaji wa Mashauri katika Mkoa wa
Iringa inaridhisha na kufafanua kuwa kwa upande wa Mahakama za Mwanzo ambazo
jumla yake zipo 21, hakuna kesi inayozidi miezi sita (6) katika Mahakama hizo.
Akiongelea katika ngazi
ya Mahakama za Wilaya, Mhe. Ngunyale alisema kuwa Mahakama hizo zina jumla ya
kesi 12 za mlundikano (ambazo zimezidi umri ya miezi 12 Mahakamani), huku kesi
8 zikiwa ni za Jinai na nne (4) zikiwa ni kesi za Madai.
Hakimu Mkazi Mfawidhi,
Mahakama ya Hakimu Mkazi-Iringa, Mhe. David Ngunyale
Mtendaji wa
Mahakama-Kanda ya Iringa, Bw. Elvin Mwakajinga
Afisa Tawala, Mahakama ya Hakimu Mkazi/Mkoa-Iringa,
Bi. Dorice Kisanga akionesha maboksi ambapo mafaili ya kesi zilizomalizika yalipohifadhiwa,
kwa urahisi wa rejea ya kumbukumbu za kesi za nyuma.
Muonekano wa jengo la Mahakama Kuu-Kanda ya Iringa,
katika uwanja huu, yapo pia majengo ya Mahakama ya Wilaya na Mahakama ya Hakimu
Mkazi-Iringa. Kwa habari zaidi BOFYA HAPA
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...