Na Mary Gwera, Mahakama, Njombe
JAJI Mfawidhi, Mahakama Kuu, Kanda ya Iringa, Mhe. Mary Shangali ametoa wito kwa Mahakimu na wadau wa Mahakama nchini kushirikiana kwa pamoja katika kutoa huduma ya haki kwa wananchi.
Aliyasema hayo mapema Juni 07, 2017  alipokuwa akiongea na Mahakimu wa Mahakama mkoani Njombe baada ya kuhitimisha ziara yake ya kukagua shughuli za Mahakama katika Mahakama za Mwanzo na Wilaya za Njombe, Ludewa na Makete pamoja na Gereza la Ludewa na Makete.
“Ushirikiano wa karibu na Wadau wa Mahakama kama Polisi, Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Mawakili na Watumishi wa Mahakama n.k  ni muhimu katika kutekeleza shughuli yetu ya utoaji haki kwa wananchi, jambo hili lina faida nyingi mojawapo ikiwa ni kusaidia kupunguza mlundikano wa kesi katika Mahakama zetu,” alifafanua Mhe. Shangali ambaye pia ni Jaji namba moja (1) wa Mahakama Kuu ya Tanzania.
Kwa upange mwingine, Mhe. Jaji Shangali alibainisha changamoto alizokumbana nazo katika ziara yake ya kukagua shughuli za Mahakama mkoani Njombe kuwa ni tatizo kubwa la usafiri wa kuwachukua Mahabusu kutoka Magerezani na kuwarudisha.
“Hii ni moja ya changamoto kubwa niliyokumbana nayo katika Mahakama zote nilizozitembelea mkoani Njombe, changamoto hii haiihusu Mahakama moja kwa moja ipo chini ya Jeshi la Polisi, lakini kwa kuwa tunafanya kazi kwa kutegemeana changamoto hii inatuathiri na inaweza kusababisha mlundikano wa mashauri na Mahabusu magerezani kutokana na Wahusika wa kesi kutofikishwa Mahakamani kwa ajili ya kusikiliza kesi zao kwa wakati stahiki,” alisema Jaji Shangali.
 Jaji Mfawidhi, Mahakama Kuu, Kanda ya Iringa, Mhe. Mary Shangali akisisitiza jambo alipokuwa akiongea na baadhi ya Mahakimu wa Mahakama mkoani Njombe baada ya kukamilisha ukaguzi katika Mahakama za Mwanzo na Wilaya zilizopo mkoani humo.
 Wahe. Mahakimu wakiandika baadhi ya masuala muhimu aliongelea Mhe. Jaji Mfawidhi katika kikao hicho kilichofanyika katika Ukumbi wa Mahakama ya Wilaya-Njombe mapema Juni 8.
  Mhe. Jaji Dkt. Paul Kihwelo, ambaye pia ni Mkuu wa Chuo cha Uongozi wa Mahakama-Lushoto Mhe. Jaji Dkt. Kihwelo yupo Njombe akiendelea na zoezi la vikao maalum vya kuondosha mlundikano wa mashauri linaloendelea kwa sasa.
 Hakimu wa Mahakama ya Mwanzo-Lupembe iliyopo mkoani Njombe, Mhe. Godfrey Msemwa akiuliza swali ili kupata ufafanuzi.
 Jaji Mfawidhi, Mahakama Kuu, Kanda ya Iringa, Mhe. Mary Shangali (wa nne kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Mahakimu wa Mahakama mkoani Njombe mara baada ya kika, wa tatu kushoto ni Naibu Msajili, Mahakama Kuu-Kanda ya Iringa, Mhe. Agatha Chugulu


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...