Na  Bashir  Yakub.
Wanaokopa  hela  kwenye  taasisi  za  fedha  wanatakiwa  kujua  haki  walizonazo. Haki  kabla  ya  kuchukua mkopo,  haki  wakati  wa  kuchukua  mkopo,  haki  wakati  wa  kurejesha,  na  haki  baada  ya  kurejesha au  kushindwa  kurejesha. Hautakiwi  kusubiri  taasisi  iliyokukopa  iwe ndiyo ya  kukueleze  haki  ulizonazo  bali  watakiwa ujue   haki    hizo  kwa  jitihada  zako.
Taasisi  ya  fedha  inaweza  kukueleza  baadhi  ya  haki  lakini  ni  muhali  kukueleza  haki  ambazo  wao  zinawabana. Watakueleza haki  ambazo  hazina  madhara  kwao.  Basi  yakupasa  ulijue  hili.
Masuala  ya  kuweka  rehani  ili  upate  mkopo  yanaongozwa  na  sheria  mbili.  Sheria  namba  4  ya  mwaka  1999    Sheria  ya  ardhi,  pamoja  nayo  Sheria  namba  17  Sheria  ya  rehani  ya  mwaka  2008. Humo  zimo haki  nyingi  za  mtoa  mkopo   wakadhalika  mchukua  mkopo.  Hata  hivyo  tutatizama  haki  moja  tu ya   notisi  kabla  ya  kuuzwa kwa   nyumba/kiwanja  cha  mkopaji.      

1.KUSHINDWA  KUREJESHA  MKOPO.
Kifungu  cha  127 ( 1 ) cha  sheria  ya  ardhi  kinaeleza   habari  ya  kushindwa  kurejesha  mkopo. Kifungu  kimeieleza  habari  hii  ikiwa  miongoni  mwa  mambo  ambayo  yanachukuliwa  kama ukiukwaji wa  masharti  ya  mkataba  wa  mkopo.  Mengine  ambayo  yanachukuliwa  kama  ukiukwaji  wa  masharti   ya  mkopo  ni  kuweka  rehani  mara  zaidi  ya  mmoja  kwa  taasisi  tofauti, kuuza, kupangisha  wakati  kuna  rehani  bila  taarifa   au  ridhaa kutoka  kwa  mtoa  mkopo n.k.  Hata  hivyo   haya  na  mengine  yatachukuliwa  kama  kukiuka  masharti  ya  mkopo  ikiwa  yamekatazwa  katika  mkataba  wako  na  taasisi  ya  fedha.
Pia  kwa  mujibu  wa  kifungu  hicho  kushindwa  kurejesha  mkopo  kunajumuisha  pesa  kamili  uliyoikopa,  riba, pamoja  na  makato  mengine  ambayo  yanajenga  sehemu  ya  mkopo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...