Na  Bashir  Yakub

Wapo  wazazi  wanaowakatalia  wazazi  wenzao  kuwaona  watoto/mtoto   baada  ya  kuwa  wameachana.  Wengine  hawakuachana  bali  hawakuwahi  hata kuishi pamoja  isipokuwa  walizaa  tu  lakini  yule  mzazi  anayeishi  na  mtoto  anamzuia  mzazi  mwenzake  kumuona  mtoto  husika. Basi  makala  haya  yatatizama  jambo  hili  kwa  sura  ya  sheria  zetu.  Uhalali  wake  na  uharamu  wake, hatua  unazoweza  kuchukua  na  mtazamo  wa  jumla  ikiwa jambo  hili  ni  haki  kisheria  ama  laah.
Sheria  namba  21  ya  mwaka  2009  Sheria  ya  Mtoto  ndiyo  itakayotupatia  majibu  ya  suala  hili  kwa  ujumla  wake.

1.KUMUONA  MTOTO  HUMAANISHA  NINI.
Unapotizama  kwa ujumla  sheria  ya  mtoto  hasa  vile  vifungu  vinavyozungumzia   habari  ya  kumuona  mtoto   utaona   kuwa   vinazungumzia  kumuona  mtoto  kwa  maana  ya  hatua  ya  baba  mzazi,  mama  mzazi,  au  mlezi  mwenye   mamlaka  kutembelea  eneo  alilohifadhiwa  mtoto  kwa  ajili  ya  kuonana  na  mtoto  huyo.
Haijalishi  anaumwa  au  yu  mzima,  yuko  kituo  cha kulelea  watoto  au  nyumbani  kwa  mtu, na  hali  nyingine  au  mazingira  yoyote  atayokuwemo. Pia kumuona  mtoto  si  tu  kumuonesha  mtu  kuwa  mtoto  ni  yule  halafu  basi.  Bali  kumuona mtoto  kunajumuisha   kumuona  na  kumgusa  kimwili.

2.  JE  NI  MTOTO   WA  UMRI  GANI  ANAYEONGELEWA  HAPA.
Kifungu  cha  4 cha Sheria ya mtoto  kinajibu  swali  hili.  Kifungu  kinasema  kuwa  mtu  mwenye  umri   wa  chini  ya  miaka  18  ataitwa  mtoto .  Kwa  hiyo  tunapoongelea   kumuona  mtoto    tunamaanisha  mtu  ambaye  umri  wake  uko  chini  ya  miaka  18  yaani  kuanzia  miaka  17   kushuka  chini.  Mwenye  miaka  18  kamili  si  mtoto  kwa  maana  ya  kifungu  hiki.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...