THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Balozi Seif Ali Idd aipongeza TFF

MAKAMU wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Balozi Seif Ali Idd, amempongeza Rais wa TFF Jamal Malinzi kwa kuhakikisha Zanzibar inapata uanachama wa FIFA.
"Mfikishie pongezi na shukurani zangu Bwana Malinzi kwa juhudi zake za kuhakikisha kuwa Zanzibar inapata uanachama wa FIFA", alisema Balozi Seif Idd mjini Zanzibar.
Akiongea na Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa Soka wa TFF, Derek Murusuri, katika ofisi za Baraza la Wawakilishi leo, Balozi Idd alisema Zanzibar inatambua juhudi zinazofanywa na Jamal Malinzi katika kuendeleza soka la Tanzania.
Alisema mafanikio ya Serengeti Boys kucheza AFCON ni mwelekeo mzuri wa ukuaji wa soka la Tanzania na uandaaji wa timu shindani ya Taifa.
"Tulikuwa na Mbunge mmoja wa Zanzibar aliyekuwa analipigia kelele sana suala hili. TFF imehakikisha Zanzibar inapata uanachama wa CAF na sasa tunatafuta FIFA," alisema.
Bw Murusuri alimwambia Makamu huyo wa Pili wa Rais wa Zanzibar kuwa tayari TFF imeshapeleka maombi ya Zanzibar kufikiriwa kupatiwa uanachama wa FIFA.
Alisema TFF tayari imeanza mkakati wa kuiandaa timu ya Taifa itakayatafuta kufuzu kucheza Kombe la Dunia mwaka 2026. Mtendaji Mkuu huyo ameishukuru Zanzibar pamoja na watanzania wote kwa kujitokeza kuichangia Serengeti Boys kucheza AFCON 2017 huko GABON.
Amewasihi waendelee kuuchangia mfuko wa maendeleo ya Soka ili usaidie kufanikisha maandalizi ya timu mpya ya Serengeti Boys, Ngorongoro Heroes (U20) na Kilimanjaro Warrious (U23).
Katika ziara hiyo, Bw Murusuri aliambatana na Mkurugenzi wa Tanzania Media Foundation (TMF), Bw Ernest Sungura ambapo makamu wa Rais ametoa pongezi kwa taasisi hiyo kuvisaidia vyombo vya habari vya Zanzibar na Tanzania kujenga uwezo wa utendaji wa kazi zao.

 Makamu  wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Balozi Seif Ali Idd katika mazungumzo na Mkurugenzi wa Tanzania Media Foundation (TMF), Bw Ernest Sungura katika ofisi za Baraza la Wawakilishi, Zanzibar
  Makamu  wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Balozi Seif Ali Idd katika mazungumzo na Mkurugenzi wa Tanzania Media Foundation (TMF), Bw Ernest Sungura  na Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa Soka wa TFF, Derek Murusuri, katika ofisi za Baraza la Wawakilishi, Zanzibar
Makamu  wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Balozi Seif Ali Idd akiongea na Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa Soka wa TFF, Derek Murusuri, katika ofisi za Baraza la Wawakilishi mjini Zanzibar.