Na Emmanuel Massaka,Globu ya Jamii

Jumuiya ya Kuhifadhi Qur-an Tanzania imeandaa  mashindano ya kimataifa ya kusoma Qur-an yanayotarajia kufanyika kesho siku ya Jumapili katika ukumbi wa Diamond Jubilee,ambapo Mgeni rasmi anatarajai kuwa Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Iddy. 

Akizungumza mbele ya Waandishi wa habari,Mwenyekiti wa Jumuiya ya Kuhifadhi Qur-an Tanzania Sheikh Othman Ally Kaporo amesema kuwa jumuiya hiyo imetenga kiasi cha dola za kimarekani elfu 25 kwa ajili ya washindi watakaoibuka kwenye mashindano hayo.

Sheikh Kaporo amesema kuwa mashindano hayo ya sita Kimataifa tangu waanze kuratibu, yanatarajia kuzishirikisha nchi 18 ambazo ni Kenya, Uganda, Mali, Nigeria, Algeria, South Africa, Bangladesh, Sudan, Kuwait, Libya, Djibouti, UAE, Russia Federation, USA, Yemen, UK, Dubai, Tanzania Bara na Visiwani (Zanzibar). Muhamedi Saidi 

Amesema kuwa matarajio yao yalikuwa ni ushiriki wa nchi 35 lakini baadhi yao ziliomba udhuru wa kutohudhuria kutokana na sababu zilizonje ya uwezo wao.

Sheikh Kaporo amesema mgeni wa heshima katika mashindano hayo atakuwa Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Iddy akiambatana na mlezi wa Jumuiya hiyo Alhaj Ally Hassan Mwinyi Rais mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Sheikh Kaporo ametoa wito kwa watanzania kuhudhuria mashindano hayo na kujitokeza kwa wingi ukizingatia huu ni mwezi mtukufu wa Ramadhani ambapo katika kumi la mwisho iliteremka Qur-an tukufu hivyo ni vyema wakahudhuria ili waweze kupata ujira kutoka kwa mola wao (Allah).

Mshiriki wa Tanzania Omary Abdallah Salum, ambaye amewaomba watanzania kuwaombea dua kwa wingi ili waweze kupata ushindi.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Kuhifadhisha Qur-an Tanzania, Sheikh Othman Ally Kaporo (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) leo jijini Dar es Salaam,kuhusiana na  mashindano ya kimataifa ya kusoma Qur-an ambayo yanayotaraji kufanyika siku ya Jumapili katika ukumbi wa Diamond Jubilee. kulia ni Katibu wa Kamati ya maandalizi ya mashindano hayo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...