Makamu wa
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan amezindua zoezi
la ugawaji wa mabeseni yenye vifaa tiba 200 yaliyotolewa na Ubalozi wa Kuwait
nchini kwa ajili ya wanawake wajawazito katika hospitali ya Mbagala Rangi Tatu na
Kituo cha Afya cha Mbagala Round Table katika wilaya ya Temeke mkoani Dar es
Salaam.
Lengo la
mpango huo ni kutoa mabeseni hayo zaidi ya 1,000 kwa wanawake wajawazito wasio
na uwezo kwa upande wa Tanzania Bara na Zanzibar kama hatua ya kukabiliana na
vifo vya watoto na wanawake wajawazito nchini.
Akizungumza katika
hafla ya uzinduzi wa ugawaji wa vifaa tiba hivyo, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan amesema kuwa mpango huo utasaidia
kwa kiasi kikubwa katika kupambana na vifo vya watoto na wanawake wajawazito
kwa kukosa vifaa tiba kutokana na umaskini unaowakabili.
Makamu wa
Rais Mhe Samia Suluhu Hassan amesema kwa maeneo yaliyopatiwa mabeseni yenye
vifaa tiba yahakikishe vifaa hivyo vinatolewa kwa wanawake wajawazito ambao
baadhi yao wanakata tamaa kwenda kujifungulia kwenye hospitali au kwenye vituo
vya afya kwa kukosa vifaa hivyo kwa
sababu ya umaskini.
Amesema
mkakati uliopo wa Serikali ni kuhakikisha huduma za afya nchini zinaendelea
kuboreshwa hasa huduma ya mama na mtoto ambapo kutokana na umuhimu wa sekta ya
afya Serikali imetenga fedha za kutoka katika bajeti ya mwaka 2017/2018.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mhe. Samia Suluhu Hassan pamoja na Balozi wa Kuwait nchini Tanzania wakiangalia mbabeseni yanya vifaa vya kusaidia wakina mama kujifungua yaliotolewa na Shirika la Red Crescent la Kuwait ambapo zaidi ya mabeseni 1000 yatatolewa kwa hospitali za Tanzania Bara na Zanzibar ,hospitali ya Mbagala Rangi 3 ilikabidhiwa mabeseni hayo yenye vifaa 100 pamoja na kituo cha Afya cha Mbagala Round Table nacho kilipokea mabeseni 100.
Baadhi ya mabeseni yenye vifaa vya kusaidia wakina mama wajawazito wakati wa kujifungua
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Bi.Arafa Nurdin wakati alipotembelea wodi ya wazazi ya hospitali ya Mbagala Rangi 3 kabla uzinduzi wa zoezi la kukabidhi vifaa vya kusaidia wakina mama wajawazito wakati kujifungua vilivyotolewa na Shirika la Red Crescent la Kuwait ambapo zaidi ya mabeseni 1000 yatatolewa kwa hospitali za Tanzania Bara na Zanzibar ,hospitali ya Mbagala Rangi 3 ilikabidhiwa mabeseni hayo yenye vifaa 100 pamoja na kituo cha Afya cha Mbagala Round Table nacho kilipokea mabeseni 100
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipata maelezo kutoka kwa Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Mbagala Rangi Dkt. Joseph Kiani wakati alipotembelea wodi ya wazazi ya hospitali ya Mbagala Rangi 3 kabla uzinduzi wa zoezi la kukabidhi vifaa vya kusaidia wakina mama wajawazito wakati kujifungua vilivyotolewa na Shirika la Red Crescent la Kuwait ambapo zaidi ya mabeseni 1000 yatatolewa kwa hospitali za Tanzania Bara na Zanzibar ,hospitali ya Mbagala Rangi 3 ilikabidhiwa mabeseni hayo yenye vifaa 100 pamoja na kituo cha Afya cha Mbagala Round Table nacho kilipokea mabeseni 100.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...