Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan amewaagiza Wakuu wa wilaya nchini kuchukua hatua stahiki katika kulinda na kuhifadhi mazingira katika wilaya zao ili kukabiliana uharibifu mkubwa wa mazingira kwenye misitu na vyanzo vya maji ili visikauke na kuleta athari kwa binadamu na viumbe wengine.

Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan ametoa kauli hiyo mara baada ya kukabidhiwa Taarifa ya Kikosi Kazi cha Mkoa wa Mbeya na Mkuu wa mkoa wa huo Amos Makalla kuhusu Mapendekezo ya Marekebisho ya mpaka kati ya Hifadhi ya Taifa ya Ruaha na Vijiji katika wilaya za Mbarari na Chunya - Ikulu, Jijini Dar es Salaam.

Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan amesema tatizo la uharibifu wa mazingira katika baadhi ya wilaya nchini ni kubwa hivyo kuna umuhimu mkubwa kwa Wakuu wa wilaya kwa ushirikiano na watendaji wengine katika kukabiliana na hali hiyo kwenye maeneo yao.

Amesema kabla ya hatua kuchukuliwa ni vizuri wananchi wakaelimishwa kuhusu umuhimu wa uhifadhi wa mazingira kabla ya kuondolewa kwenye maeneo waliyovamia ikiwemo maeneo ya vyanzo vya maji.

Makamu wa Rais pia amepongeza timu ya wataalamu wa kikosi kazi cha Mkoa wa Mbeya kwa kazi kubwa na nzuri waliyoifanya inayolenga kuokoa mfumo wa ikolojia katika Bonde la Mto Ruaha Mkuu.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipokea taarifa kutoka kwa Mkuu wa mkoa wa Mbeya Ndugu Amos Makala ya kikosi kazi cha mkoa wa Mbeya kuhusu mapendekezo ya marekebisho ya mpaka kati ya Hifadhi ya Taifa ya Ruaha na Vijiji kati ya Wilaya ya Mbarali na Chunya (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimsikiliza Mkuu wa mkoa wa Mbeya Ndugu Amos Makala wakati wa uwasilishwaji wa taarifa ya kikosi kazi cha mkoa wa Mbeya kuhusu mapendekezo ya marekebisho ya mpaka kati ya Hifadhi ya Taifa ya Ruaha na Vijiji kati ya Wilaya ya Mbarali na Chunya (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza mbele Mkuu wa mkoa wa Mbeya Ndugu Amos Makala pamoja na kikosi kazi chake wakati wa uwasilishwaji wa taarifa ya kikosi kazi cha mkoa wa Mbeya kuhusu mapendekezo ya marekebisho ya mpaka kati ya Hifadhi ya Taifa ya Ruaha na Vijiji kati ya Wilaya ya Mbarali na Chunya (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...