Na Karama Kenyunko, blogu ya jamii.

MAKAMU wa Rais, Samia Suluhu Hassan amewataka waendesha mashitaka, polisi na wapelelezi wa kesi za wanyamapori na misitu kubadilika katika kazi zao ili kulinda rasilimali hizo kwa vizazi vya sasa na vijavyo.Aidha, ameitaka mahakama kutoa muongozo kwa watumishi wake kuhusu namna ya kuendesha kesi zinazohusiana na nyara za serikali kwa lengo la kuwa na uwiano sawa katika utoaji amri.

Samia amesema hayo leo mjini Dar es Salaam wakati wa uzinduzi wa Mwongozo kwa wapelelezi, waendesha mashitaka na Polisi wa kesi za wanyamapori na misitu ulioandaliwa na Mkurugenzi wa Mashitaka nchini (DPP).

Amesema wote hao wanatakiwa kufanya kazi zao ipasavyo kuhakikisha usalama wa wanyamapori na misitu kwani kwa kupoteza maloiasili hizo kunafanya uchumi wa nchi kushuka na kwamba wasifanye kazi hiyo kwa kuweka mazingira ya rushwa.

Amesema, kazi za kupeleleza na kuendesha kesi za wanyamapori zimekuwa na ushawishi mkubwa wa rushwa kutoka kwa wahusika na kuwataka kufikiria maslahi mapana ya nchi na sio wao binafsi.

"Jamani, msiogope kufa, kifo kipo na kila mmoja wetu atakufa hata mnyama ikiwemo huyo FaruJohn, muhumu ni namna ya kujua aina ya kifo utakachokufa, lakini Jambo la kusikitisha mmekuwa mkiponzwa na fedha, wahenga walisema 'fedha ni sabuni ya roho lakini pia walisema fedha ni fedheha," amesema Samia.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu  Hassan akikata utepe kuashiria Uzinduzi Kitabu cha Mwongozo kwa Wapelelezi na Waendesha Mashitaka wa Kesi za Wanyamapori na Misitu kwenye ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam, wengine pichani ni Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Profesa Jumanne Maghembe (kulia),Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Bw.  Alvaro Rodrigues na kushoto ni Muendesha Mashtaka Mkuu wa Serikali Biswalo Mganga na Naibu wa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhandisi Hamad Masauni (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais - Ikulu) Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimkabidhi Naibu wa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhandisi Hamad Masauni Kitabu cha Mwongozo kwa Wapelelezi na Waendesha Mashitaka wa Kesi za Wanyamapori na Misitu kwenye ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam, katikati ni Muendesha Mashitaka Mkuu wa Serikali Biswalo Mganga. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais - Ikulu)Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu  Hassan akihutubia wakati wa Uzinduzi wa Mwongozo kwa Wapelelezi na Waendesha Mashitaka wa Kesi za Wanyamapori na Misitu kwenye ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais - Ikulu).

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...