Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan
amewaagiza waajira wasiopeleka au kuchelewesha michango ya wanachama
kwenye mifuko ya hifadhi ya jamii nchini wachukuliwe hatua za kisheria
ili kukomesha tabia hiyo.
Makamu
wa Rais ametoa kauli hiyo 3-June-2017 Jijini Mwanza wakati anafungua
semina ya maisha baada ya kustaafu,fursa ya mafao,uwekezaji
iliyoandaliwa na Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma (PSPF) kwa
ajili ya wastaafu watarajiwa 450 kutoka wilaya zote za mkoa wa Mwanza.
Makamu
wa Rais amesisitiza kuwa waajiri wakichangia kwa mujibu wa sheria
kwenye mifuko hiyo watawezesha wanachama wao kupata mafao kikamilifu na
kwa wakati.
Kuhusu
madeni ya Serikali kwa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii nchini, Makamu wa
Rais amewahakikishia Wakurugenzi wa mifuko hiyo kuwa Serikali
inashughulikia madeni hayo na baada ya kukamilika kwa zoezi la uhakiki
wa madeni hayo basi malipo yatafanyika haraka iwezekanavyo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia wakati wa ufunguzi wa Semina kwa wastaafu watarajiwa iliyofanyika kwenye ukumbi wa Benki Kuu jijini Mwanza
Baadhi ya washiriki wa Semina ya Wastaafu Watarajiwa wakisikiliza kwa makini hotuba ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan iliyofanyika kwenye ukumbi wa Benki Kuu Mwanza.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akionyesha Vitabu vya PSPF kwenye kutoa elimu kwa Wanachama wa mfuko huo.
Baadhi ya washiriki wa Semina ya Wastaafu Watarajiwa wakisikiliza kwa makini hotuba ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan iliyofanyika kwenye ukumbi wa Benki Kuu Mwanza.
Baadhi ya Wadau wakifuatilia ufunguzi wa Semina kwa Wastaafu Watarajiwa.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...