THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

MAKAMU WA RAIS SAMIA SULUHU HASSAN AKABIDHIWA VIFAA TIBA VYA UZAZI ZAIDI YA 200 NA BALOZI WA KUWAIT HAPA NCHINI

Balozi wa Kuwait hapa nchini Jasem Al- Najem amemkabidhi Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan vifaa tiba vya uzazi zaidi ya 200 ambavyo vitasambazwa katika hospitali mbalimbali kwa Tanzania Bara na Zanzibar.

Makabidhiano ya vifaa hivyo vya uzazi yamefanyika leo Ikulu ya Dar es Salaam ambapo Balozi wa Kuwait hapa Nchini Jasem Al- Najem amesema Serikali ya nchi hiyo imetoa vifaa hivyo kama hatua ya kuendelea kudumisha na kuendeleza mahusiano mazuri kati ya nchi hiyo na Tanzania.

Amesema kuwa Serikali ya Kuwait imetoa vifaa hivyo ikiwa ni awamu ya kwanza na lengo ni kutoa vifaa hivyo zaidi ya 1000 vyenye thamani ya shilingi milioni 40 kwa wanawake wajawazito na waliojifungua katika hospitali mbalimbali nchini.

Mara baada ya kupokea msaada huo, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan ameishukuru Serikali ya Kuwait kwa msaada huo ambao utasambazwa katika hospitali mbalimbali kwa Tanzania Bara na Zanzibar.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA.


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipokea beseni lenye vifaa vya uzazi kutoka kwa Balozi wa Kuwait nchini, Jasem Al-Najem.Kuwait imetoa mabeseni 200 ya vifaa vya uzazi kwa hatua ya awali ambapo watatoa zaidi ya mabeseni 1000 yenye vifaa vya uzazi. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais).
Makamu wa Rais Mhe.Samia Suluhu Hassan akitazama moja ya Dawa,mara baada ya kukabidhiwa mapema leo Ikulu jijini Dar,vifaa tiba vya uzazi zaidi ya 200 na Balozi wa Kuwait hapa nchini,Mhe,Jasem Al-Najem,vifaa hivyo vitasambazwa katika hospitali mbalimbali kwa Tanzania Bara na Zanzibar.